• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kupunguza miundo ya serikali na kufanya ugatuzi wa madaraka

    (GMT+08:00) 2013-03-01 19:20:33

    Mkutano wa wajumbe wa chama cha kikomunisti cha China umeidhinisha mpango wa kupunguza miuundo na madaraka ya serikali kuu. Mpango wa mageuzi ya miundo ya serikali unatarajhiwa kuwasilishwa kwenye mkutano ujao wa bunge la umma la China.

    Taarifa iliyotolewa na mkutano huo inasema mageuzi hayo ya serikali yamesanifiwa kujaribu kuunda serikali "rahisi zaidi na yenye kugatua madaraka'. Taarifa hiyo inasema kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China imedhamiria kuimarisha usafi na ufanisi wa serikali. Baada ya mkutano wa siku tatu wa kamati kuu ya chama, katibu mkuu wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China CPC Bw Xi Jinping alisema mabadiliko hayo ya serikali yatasaidia kuondoa vikwazo vya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hayo ni mabadiliko makubwa ya idara za serikali kufanywa katika kipindi cha miaka 30 iliyopita. Professor Zhu Lijia ambaye ni mtaalamu wa mambo ya usimamizi wa umma katika chuo cha mambo ya utawala cha China anasema mabadilkiko haya mapya yanatokana na mambo ambayo yamefanywa tangu mwaka wa 2008.

    "Kuna mambo kadhaa ambayo hayakushughulikiwa mwaka wa 2008 kama vile kutokuwa na ushirikiano na uratibu kati ya idara za serikali. Sasa wanajaribu kutatua tatizo hilo, kujenga serikali ya watu huku lengo kuu likiwa usimamizi wa soko, usimamizi wa makundi ya jamii na huduma kwa umma".

    Mkutano huo umeahidi kuendeleza mageuzi makubwa katika wizara ili kuleta ufanisi katika idara zake. Professa Zhu Lijia anasema mageuzi ya sasa ya wizara yatakuwa na manufaa katika kufafanua majukumu ya idara za serikali

    "mageuzi yanalenga kufafanua mipaka ya utungaji sera, utekelezaji wa sera na usimamizi. Tatizo la sasa ni kuwa idara nyingi za serikali ni watungaji sera, watekelezaji na wasimaizi. Sio vigumu kuelewa kuwa hii ndio inayosababaisha ufanisi mdogo".

    Wizara 15 za serikali zilihusika katika mabadiliko ya mwaka wa 2008. Wakati huu, idara za kulinda usalama wa chakula zitaunganishwa kuwa wizara inayojumuisha majukumu ya usimamizi, na wizara ya reli itaunganishwa na wizara ya mawasiliano na uchukuzi. Pamoja na mabadiliko hayo ya wizara, serikali kuu pia inawajibu wa kuhamishia baadhi ya majumuku yake katika ngazi za chini za serikali, na mashirika ya kijamii.

    Taarifa hiyo imesema, hayo yatatekelezwa kwa kutenganisha zaidi utawala wa serikali kutoka kwenye makampuni, uwekezaji, mambo ya kijamii na usimamizi wa makundi katika jamii. Profesa Zhu Lijia anasema huu ni mwanzo wa mabadiliko.

    "China ya sasa inahitaji serikali itakayogatua madaraka na mashirika ya kijamii yenye nguvu. Huu ndio mwelekeo sahihi wa serikali katika kuhakikisha kiwango cha maendeleo ya kijamii na kuboresha maisha ya watu. Serikali kuu inatakiwa kupunguza madaraka yake na kufafanua majukumu yake".

    Miongo mitatu ya mageuzi nchini China yamepunguza idadi ya idara za serikali kuu za serikali kutoka 53 hadi 27 pamoja na kuondoa karibu mashirika 30 yaliyo na uhusiano na baraza la serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako