• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kwanza wa bunge la awamu mpya la umma la China wafunguliwa hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2013-03-06 10:01:28

    Mkutano wa kwanza wa bunge la awamu mpya la umma la China umefunguliwa tarehe 5 hapa Beijing. Bunge hilo likiwa ni chombo chenye madaraka ya juu nchini China, litachagua na kuamua miundo ya serikali ya awamu mpya ya China. Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao siku hiyo ametoa ripoti ya kazi za serikali kwenye mkutano huo akisisitiza kuwa mageuzi na ufunguaji mlango ni nguvu ya kimsingi ya kusukuma mbele maendeleo ya China, China inapaswa kuwa na ushupavu na burasa zaidi za kisiasa ili kusukuma mbele zaidi mageuzi na ufunguaji mlango.

    Ripoti yake hiyo inajumuisha kazi za miaka mitano iliyopita, kutoa matakwa ya jumla, malengo makuu na sera za jumla za uchumi kwa maendeleo ya jamii na uchumi kwa mwaka huu, na pia inatoa mapendekezo kwa kazi za serikali ya awamu mpya.

    Baada ya utekelezaji wa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango kwa zaidi ya miaka 30, juhudi za kuwafanya wananchi wanufaike na mafanikio yaliyopatikana zimepewa kipaumbele na serikali. Bw. Wen Jiabao akisema:

    "tunatilia mkazo kazi ya kuongeza nafasi za ajira katika juhudi za kuhakikisha na kuboresha maisha ya wananchi, katika miaka mitano iliyopita, serikali imewekeza yuan bilioni 197.3, ambazo zimesaidia wahitimu milioni 28 wa vyuo vikuu na wakazi milioni 8.3 wa mijini wasio na ajira wapate ajira. Wakazi wote wa mijini wananufaika na bima ya matunzo ya uzeeni. Mfumo wa huduma za matibabu za kimsingi umekamilika kwa hatua ya mwanzo, ambao unashirikisha watu bilioni 1.3 kwa bima za matibabu za aina mbalimbali. Serikali pia imejenga na kukamilisha utaratibu wa kuhakikisha wakazi wa mijini wenye matatizo ya kiuchumi wanapata nyumba ya kuishi, na eneo linalotekeleza utaratibu huo linapanuliwa hatua kwa hatua."

    Kwenye mkutano, wajumbe wanajadili kwa makini malengo ya utawala wa serikali ya China. Kwenye mitaa ya mjini Beijing, watu wanaofuatilia mkutano huo pia wameeleza matarajio yao kuhusu maisha bora.

    "vyakula, burudani, na kila kitu kingine vyote vinapatikana, wazee wanatunzwa, kiwango cha maisha kiko sawa. Tunaridhika na hali ya sasa, na tunatarajia maisha bora zaidi."

    Natarajia sera za serikali zitatunufaisha zaidi, natarajia kununua nyumba yangu mwenyewe."

    Katika miaka mitano iliyopita, China imekabiliana na changamoto nyingi zikiwemo msukosuko wa fedha duniani na tetemeko kubwa la ardhi la Wenchuan. Pia katika kipindi hicho, pato la taifa GDP la China limechukua nafasi ya pili duniani. Hata katika hali ya kudidimia kwa uchumi duniani, uchumi wa China pia umebadili mwelekeo wa kushuka na kuweka msingi mzuri kwa mwaka huu. Lakini Bw. Wen Jiabao pia amekiri kuwa, matatizo ya kutokuwepo kwa uwiano wa maendeleo, na maendeleo yasiyo ya endelevu, bado ni makubwa.

    Ili kukabiliana na hali ya uchumi yenye changamoto kubwa, Bw. Wen Jiabao ametoa lengo la asilimia 7.5 la ongezeko la uchumi kwa mwaka huu, serikali itaendelea kutekeleza mambo ya fedha kwa hatua madhubuti, ili kutimiza maendeleo mazuri ya endelevu ya uchumi.

    Kwa mujibu wa katiba ya China, kipindi cha kila awamu ya serikali kiko sawa na kile cha bunge la umma, na viongozi hawawezi kuwa madarakani kwa zaidi ya vipindi viwili. Bw. Wen Jiabao amekuwa waziri mkuu wa China tangu mwaka 2003, na kwa ujumla ametoa ripoti 10 za kazi za serikali, ingawa ripoti ya mwaka huu ni fupi, lakini imebeba mageuzi na matumaini yaliyojumuishwa ya miaka 10 iliyopita. Kwa kutupia macho siku za baadaye, China itatilia maanani zaidi kutoa kipaumbele kwa maslahi ya watu, na kujitahidi kutimiza maendeleo endelevu kwa pande zote na yenye uwiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako