• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0305

    (GMT+08:00) 2013-03-11 14:40:38
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Yohana Marwa, wa clabu ya wanakemogemba S.L.P 71 Tarime Mara Tanzania, naye anasema ninayofuraha kubwa kutumia nafasi hii kuungana na Ndugu zetu wananchi wa China kwa muda huu wanapoadhimisha sherehe zao za mwaka mpya wa kichina. Hakika ni furaha sana pale kila mtu anapomaliza mwaka akiwa mzima salimini. kweli ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu.

    Ijapo kuwa ni mda mrefu kidogo nimekuwa kimya lakini napenda kuwahakikishia kuwa niko pamoja nanyi katika kusikiliza matangazo ya CRI pale yanapokuwa hewani, kwani sikubali kuukosa uhondo wa matangazo ya CRI kwa sababu kuna mengi sana ninanufaika nayo kwa kuisikiliza idhaa hii ya kiswahili kulingana na jinsi inavyotujali sisi wasikilizaji wake popote pale tunapoitegea sikio, kwa nyakati mbalimbali hivyo basi ndio maana najivunia idhaa hii bila kujali niko maeneo gani. Sina mengi isipokuwa kuwatakia kila la heri katika shughuli zenu za kila siku na Mungu awabariki.

    Nasi pia tunakushukuru sana msikilizaji wetu Yohana Marwa kwa barua yako, tunashukuru siku kuu ya mwaka mpya tulisherehekea vizuri na salama na hivi sasa baada ya mapumziko ya wiki moja tumerejea kazini ili kuliendeleza taifa la China, ahsante sana.

    Sasa ni zamu ya msikilizaji wetu Choma wa Choma ama Kamanda Wa Mashambulizi ya Salamu wa S.L.P 108 Mwamkulu Mpanda Tanzania anasema kwanza salamu zangu ziwafikie watangazaji, wa CRI, mimi nawapogeza kwa kutuletea matangazo yenu hapa barani Afrika, ila tunataka matangazo tuyapate hapa Tanzania sio kupitia KBC, asanteni kwa matangazo ya uhakika. Pia nawapongeza kwa kuadhimisha sikukuu ya jadi ya kichina lazima jadi isisahauliwe, kwani sio vizuri. Hata na sisi hapa Tanzania bado tunakumbuka mila na desituri nawapogeza wachina.

    Kwanza tunakushuru sana msikilizaji wetu Choma Wa Choma kwa barua yako, pili tunapokea pongezi za maadhimisho ya sikukuu kwa mikono miwili kwani safari hii sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China ilifana sana na wachina wote walifurahia na kusherehekea kama kawaida, asante sana.

    Barua ya mwisho iantoka kwa msikilizaji wetu Mbarouk Msabah Mbarouk wa S.L.P 906 AL Hamriya PC131 Muscat Oman, anasema napenda kutoa pongezi zangu nyingi kwa mfanyakazi na mtangazaji mkongwe zaidi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI Bibi Chen Lianying anayejulikana zaidi hewani kwa jina la " Mama Chen " kwa kufaulu kuwa miongoni mwa Wachina 10 waliopewa tuzo kwa mchango wao mkubwa kwa ajili ya urafiki kati ya Jamhuri ya Watu wa China na Afrika, katika sherehe zilizofanyika mjini Beijing hapo tarehe 21 December mwaka uliopita wa 2012.

    Bila shaka kwetu sisi wasikilizaji wa zamani wa Idhaa hii na hata wale wa sasa pia tunatambuwa vyema juhudi, bidii na harakati kubwa za Mama Chen katika kuikuza na kuiendeleza dhamira ya kuboresha uhusiano wa Kirafiki kati ya China na Afrika kupitia daraja hili la Lugha ya Kiswahili inayotangazwa hewani kupitia CRI, kwani licha ya kwamba Mama Chen aliwahi kusomea lugha ya Kiswahili barani Afrika na kufanya ziara za mara kwa mara za kuwatembelea wasikilizaji katika maeneo mbali mbali ambako vipindi vya Idhaa hii vinasikika, lakini pia amekuwa ni nguzo muhimu kwa Watangazaji chipukizi wa Kichina katika Idhaa ya Kiswahili ya CRI kutokana na uzoefu wake na kipaji chake cha muda mrefu .

    Hivyo juhudi za Mama Chen zimestahiki vyema kuheshimiwa na kutukuzwa, hivyo tuzo aliyopokea imekuwa ni fahari kubwa kwake, kwetu sisi na kwa Radio China Kimataifa kwa ujumla. Mwisho ningependa kumtakia kila la kheri, afya njema na maisha marefu Bibi Chen Lianying na kamwe hatutaweza kusahau juhudi na bidii zako za kuendeleza na kukuza urafiki kati ya Afrika na Jamhuri ya Watu wa China. Ahsanteni sana.

    Nami nakushukuru kwa moyo wa dhati msikilizaji wetu Mbarouk Msabah Mbarouk kwa barua yako, kwa kweli naingia moyo ninaposikia wasikilizaji mbalimbali wakitoa maoni yao kuhusu ushindi niliopata, kwani hii inathibitisha kuwa kweli juhudi zangu zinathaminiwa na zitaendelea kuthaminiwa hata kama nitaondoka CRI, nashukuru sana na nasema tupo pamoja katika kuendeleza na kukuza urafiki kati ya China na Afrika, asnate sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako