• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0312

    (GMT+08:00) 2013-03-11 14:41:33
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Mutanda Ayubu Sharifu wa S.L.P 172, Bungoma Kenya anaanza kwa kusema pokeeni salamu za dhati, nikiwafahamisha kuwa nimewamiss wote kwa muda, kwani ni muda tangu niandike barua kwa idhaa ya Kiswahili ya CRI. Kwasababu idhaa hii ndiyo iliyoniwezesha kuvuka mito, miamba, mabonde na milima pamoja na ziwa kubwa duniani na vyote vilivyomo ulimwenguni. Kupitia shirika la ndege la Kenya 'Airways' KQ, Dubai emirates na 'China, Chinese airlines' au Southern China.

    Bila kusahau treni ya kasi kama upepo. Niliweza kusafiri kwa muda mfupi kutoka Beijing mpaka Shanghai na kushuhudia jinsi China ilivyonawiri kwa viwanda na utaalamu wote duniani. Katika mji huo wa Shanghai ambako kuna kila kitu na ujenzi wake ni wa usiku na mchana. Shukrani zote ziende kwa wakurugenzi wa shirika la habari la CRI.

    Kando na hayo makaribisho ya hali ya juu, kutoka kwa wafanyakazi wa CRI Swahili Service, zawadi tele nilipokea. Niliweza kuzuru, kula na kunywa katika hoteli za hali ya juu. Nilivyoendelea kutazama michezo ya sanaa na hali ya teknolojia, akili yangu iliweza kusimama kwa muda wa dakika kumi na kutafakari mengi, kwani matarajio yangu ya maisha nchini China yalikua tofauti. Kama kawaida mwafrika anapotembelea nchi iliyostawi huwa na mawazo au fikira tofauti kabisa, kwani wengi huamini ni wakati wao wa kutajirika kwa kupewa mali ya haraka. La hasha!, katika nchi ya China utaweza kupata ujuzi na kupatanisha mawazo na baada ya kuweka bidii maishani utafaulu vizuri sana na kwa ustadi. Kwa hivyo changamoto niliyopewa ni kufanya kazi kwa bidii, kuvumilia na panapokuwa na nia pana njia. Mimi naona maisha yangu yakibadilika mara kwa mara kama vile maziwa hubadilisha maji na kuwa na rangi nyeupe pepepe

    Sasa ninaweza kujigamba kwamba baada ya miaka saba, maisha yangu yanaendelea kuboreshwa na hali yangu yaendelea kuimarika. Hii ni kwa sababu tu ya yale yote niliyoweza kuyaona ana kwa ana. Ingawa walionishuku nawaonya kuwa waendelee kusubiri kidogo tu nitawashangaza kwa mambo mengi, kwani mabadiliko hayaji kwa Ghafla kama vile nchi za magharibi mara kwa mara huwa zinatumia mbinu ya kujitajirisha baada ya waafrika bila kuwapa mwelekeo wa kutunza mali. Hii ni kama kumpa mtu samaki badala ya kumpa ndoano ili ajishughulishe mwenyewe.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Mutanda Ayubu Sharifu kwa barua yako, kwa kweli tunafurahia sana kuona kuwa bado una kumbukumbu nzuri ya China, na kila ulilofanyiwa upokuwa huku, ila tunatumai sasa utakuwa na muda wa kutuandikia baada ya kimya cha muda mrefu ahsante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Ras Franz Manko Ngogo wa S.L.P 71 Tarime, Tanzania anasema Licha ya kuizuru hii tovuti, napenda kuwapa mkono wa pongezi watu wote wanaoisikiliza hii idhaa. Sababu kuu ikiwa ni zawadi na tuzo tulopata watu wa Kiswahili kwa Mama yetu mwenye Moyo na upendo kwa kila mtu; Mama Chen, kubeba hilo joho miongoni mwa watu 10 tu. Ni wazi kuwa alistahili nafasi hiyo kwa bidii na jitihada alizofanya kuhakikisha kuwa urafiki Kati ya China na Afrika unasonga mbele. Binafsi namuunga mkono na niliyapokea matokeo hayo kwa furaha sana. Tunapaswa kumfanyia sherehe maalumu sisi wasikilizaji na watangazaji wa CRI. Naomba hilo lijadiliwe na kuungwa mkono. Ahsante.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Ras Franz Manko Ngogo kwa barua yako fupi, kwa kweli hata sisi pia tumefurahia na tunajivunia kwa ushindi nilioupata, lakini kukujibu kuhusu kuandaliwa sherehe itakayowashirikisha wasikilizaji na watangazaji, kwa sasa haitawezekana kwani siku ya kupokea tuzo tuliandaliwa sherehe kubwa kwa hiyo tunaomba radhi kwa hilo,ahsante sana.

    Naye msikilizaji wetu Xavier Lincolyn Telly-Wambwa wa S.L.P 1993-50200, Bungoma Kenya anasema Wanawake ni viumbe vya kuheshimiwa sana. Wana moyo wa huruma sana na ninajivunia kwa sababu marehemu mamangu mzazi alijitolea kunilea na ndio maana hivi leo nipo hivi nilivyo. Wanawake ni watu wa heshima zaidi kuliko sisi wanaume. Mke wangu au wake zetu wanatujali kwa upendo na mapenzi moto moto. Kwani chakula kitamu chatokana na furaha waliyonao na bila shaka furaha yao ni asilimia 100. Wana ukarimu wa hali ya juu na urembo wa kuvutia na nidhamu. Asante

    Kwa niaba ya wanawake wote nakushukuru kwa dhati ya moyo wetu Bw. Xavier Lincolyn Telly-Wambwa kwa barua yako ambayo inaonesha kuwajali sana wanawake, kwa vile juzi tu tuliadhimisha siku ya wanawake duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni kuzuia vitendo vya kikatili kwa wanawake, tunaposikia wanaume wakitoa mchango kama huo tunajua kuwa juhudi zetu wanawake zinazaa matunda sana, tunakushukuru sana.

    Na barua ya mwisho inatoka kwa Bw Mogire Machuki wa kisii Kenya baruapepe yake ni oscarmogire@yahoo.com anasema habari rafiki zangu. Ni furaha kwangu kuwa hatimaye KBC TV imeanza kurusha hewani mchezo wa kuigiza wa Doudou na Mama Wakwe Zake kila siku ya jumapili jioni. Ni afueni kwetu kuwa CRI imefanikisha mpango huu, bado nafuatilia tamthilia maarufu. Shukrani.

    Nasi tunakushuru pia kwa barua fupi sana, tumefanya hivyo ili kutimiza lengo la kuweka usawa kwa nchi za Afrika Mashariki kwani nyote tunawajali, ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako