• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujenzi wa utaratibu ni msingi katika mapambano dhidi ya ufisadi

    (GMT+08:00) 2013-03-11 17:50:22

    Mikutano ya mwaka wa bunge la umma na baraza la mashauriano ya kisiasa la China inaendelea hapa Beijing. Uchunguzi uliofanywa na vyombo vya habari unaonesha kuwa, ufuatiliaji kuhusu suala la mapambano dhidi ya ufisadi umeendelea kuchukua nafasi ya mbele kwa miaka kadhaa mfululizo.

    "China inapaswa kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi, kuimarisha ujenzi wa maadili ya serikali, na kubadilisha kwa mujibu wa utazratibu hali ambayo madaraka yanamilikiwa zaidi kwenye idara au watu bila usimamizi na udhibiti wa kutosha, ili kuhakikisha kwamba makada waweze kuondokana na ufisadi, serikali zitafuata nidhamu na maadili".

    Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao alisema hayo alipozungumzia suala la mapambano dhidi ya ufisadi kwenye ripoti yake kuhusu kazi za serikali. Matumizi ya ovyo ya madaraka, fedha na magari ya serikali ambayo yametokea kutokana na kutokuwa na udhibiti wa madaraka yanafuatiliwa na wananchi wengi zaidi. Kauli iliyotolewa na kiongozi mpya wa chama cha kikomunisiti cha China Bw. Xi Jinping kuwa "ni lazima madaraka yatumiwe kwa mujibu wa utaratibu," imekaribishwa na watu wa sekta mbalimbali katika jamii ya China. Mjumbe wa mkutano wa bunge la umma Bw. Li Bin alipendekeza kuwa kitu muhimu cha kuzuia matumizi mabaya ya madaraka ni kusimamia vizuri fedha, maliasili na mali za umma.

    "ni rahisi kwa matatizo kutokea katika ugawaji, usimamizi na uendeshaji wa matumizi ya mitaji ya umma, maliasili na mali za umma, kwa hiyo ni lazima kuimarisha usimamizi wa pande hizo tatu, na ujenzi wa utaratibu husika, kwanza China inapaswa kufanya uchunguzi wazi kuhusu pande hizo tatu, halafu kuhakikisha shughuli zote zinafuata utaratibu kwenye msingi huo."

    Mjumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Gan Yisheng alisema, ni lazima kuunganisha ujenzi wa utaratibu wa kuzuia ufisadi na mageuzi ya mfumo wa mambo ya utawala, ili kuweza kupanga, kuzuia na kusimamia madaraka kwa kufuata utaratibu.

    "kazi ya kujenga na kukamilisha utaratibu si kama tu inapaswa kufuata uzoefu mzuri wa zamani, na bali pia inapaswa kuiga uzoefu wa nchi nyingine, ili kuanzisha utaratibu wenye ufanisi unaolingana na hali halisi ya China."

    Mjumbe Bw. Gong Fuwen aliyefanya utafiti wa sheria kwa miaka mingi anaona kuwa, China inapaswa kuimarisha kazi za kutunga sheria kuhusu kuzuia, kutoa adhabu na kuzuia ufisadi, ili kupambana na ufisadi kisheria.

    Mbali na Bw. Gong Fuwen, pia kuna wajumbe wengi wanaofuatilia utungaji wa sheria husika, na mapendekezo yao yamepata jibu. Naibu mkurugenzi wa kamati ya masuala ya sheria ya katika Halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la China bw. Lang Sheng hivi karibu amesema, katika miaka mitano ijayo, bunge hilo litaanza kazi za kukamilisha utungaji wa sheria ya kupambana na ufisadi, ili kuunda utaratibu kamili wa kuadhibu na kuzuia ufisadi.

    Ripoti ya kazi ya mahakama kuu na idara kuu ya uendeshaji mashtaka ya China hivi karibu zimefikishwa kwenye bunge la umma. Ripoti hizo mbili zinaonesha kuwa, katika miaka ya hivi karibuni idara za utekelezaji sheria za China zimeongeza nguvu zaidi katika mapambano dhidi ya ufisadi. Mkuu wa idara kuu ya uendeshaji mashtaka ya China Bw. Cao Jianming alisema, idara hizo zitaendelea kusukuma mbele ujenzi wa maadili ya serikali na mapambano dhidi ya ufisadi, ni lazima zihakikishe kuwa matukio yote yanachunguzwa, na wahusika wote wa ufisadi wanachukuliwa hatua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako