• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyuo vya Confucius kuanzishwa katika miji mikubwa 500 duniani ifikapo mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2013-03-11 17:54:57

    Vyuo vya Confucius vinatarajiwa kuanzishwa katika miji mikubwa 500 duniani ifikapo mwaka 2020, na vitachangia kueneza lugha ya kichina sehemu mbalimbali duniani.

    Hayo yamesemwa leo tarehe 11 na katibu mkuu wa makao makuu ya vyuo vya Confucius ambaye pia ni mkurugenzi wa Ofisi ya taifa ya lugha ya kichina Bibi Xu Lin. Ameongeza kuwa, hadi sasa China imepeleka walimu na watu wa kujitolea wapatao elfu 10 katika vyuo hivyo. Aidha, amesema idadi ya walimu wenye kiwango cha juu ni ndogo, vitabu vinavyofaa kwa mafunzo ni vichache, na kiwango cha utoaji wa mafunzo kinahitaji kuongezwa.

    Katika kipindi kijacho, vyuo vya Confucius vitaweka mkazo katika kuanzisha vituo vya kuwaandaa walimu na watu wa kujitolea, kuharakisha kazi ya kuandaa vitabu vya mafunzo ya kichina vinavyoandikwa kwa lugha mbalimbali, na kuimarisha ujenzi wa vyuo vya Confucius katika mtandao wa Internet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako