• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuhudumia familia zilizopoteza mtoto wao wa pekee

    (GMT+08:00) 2013-03-13 19:36:13

    Tatizo kubwa linaloikumba jamii ya China hivi sasa ni jinsi ya kuwatunza wazee ambao watoto wao wamefariki. Kama inavyojulikana, hapa China kuna sheria ya kuwa na mtoto mmoja tu kwa familia moja. Sasa kama mtoto huyo amefariki, wazazi wake wanatunzwa na nani? Wazazi hao wanajikuta wakikabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi, kisaikolojia, na ya kijamii.

    Kutokana na sheria ya kuwa na mtoto mmoja tu kwa familia moja iliyopitishwa hapa China mwaka 1979, mamilioni ya familia zimefuata sheria hiyo. hivyo kuwa na mtoto mmoja tu. Kama familia hizo zikipoteza mtoto huyo, au mtoto huyo akipata ulemavu baada ya umri wa wazazi kupata mtoto mwingine kupita, familia za wazazi hao zitakuwa "Shi Du Jia Ting", tafsiri ya moja kwa moja ni "familia zilizopoteza mtoto wao wa pekee". Katika miaka ya karibuni, idadi ya familia hizi imeongezeka kwa kasi hapa China. Kutokana na kipato kidogo kinachosababishwa na kutokuwa na hali nzuri ya kimwili na kiafya, maisha ya wazee hawa yamekuwa ya upweke na ya kukata tamaa.

    Profesa Wang Ming wa Chuo Kikuu cha Tsinghua alianza kufuatilia kwa makini hali ya kundi hili la wazee alipokuwa akiandika mapendekezo ya kuishauri serikali ifanye marekebisho ya sera ya mpango wa familia.

    "Familia ina maana gani? Familia inaundwa na wazazi na mtoto wao. Mtoto anawakilisha matumaini na matarajio ya siku za baadae. Familia iliyopoteza mtoto wao ni kama familia iliyopoteza matarajio ya baadae na matumaini"

    Wang Ming anaona kuwa, tatizo linatokana na sera ya kipekee ya familia ya taifa, hivyo serikali inatakiwa kubeba jukumu la kulisaidia kundi hili. Wang pia amependekeza kuwa serikali irekebishe sheria ya "kupanga mtoto" (adoption) ili kuwapa tumaini na kuwaunga mkono familia hizo "kupanga" watoto yatima kama wako tayari kufanya hivyo. Kwa familia ambazo haziko tayari "kupanga" , kifungu cha 27 cha sheria ya idadi ya watu na mpango wa uzazi kinasema kuwa, serikali za mitaa zinapaswa kutoa msaada unaotakiwa kuzisaidia familia hizo kama tayari zimevuka umri wa kupata mtoto wa pili.

    Lakini Yang Jia, mjumbe wa kamati ya mashauriano ya serikali, ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia haki za watu wenye ulemavu, anaona kuwa serikali inatakiwa kukifanyia marekebisho kifungu hicho kwa kuwa hakikueleza wazi msaada wa aina gani ni muhimu kwa familia hizo.

    "Tunatakiwa kueleza wazi msaada wa lazima unatakiwa kutoka maeneo yote matatu – kiuchumi, kisaikolojia, pamoja na huduma za afya na uzee, kama vile nyumba za kuishi wazee, ili serikali za mitaa zijui sehemu gani zinatakiwa kupewa umuhimu zaidi na mahali gani panatakiwa msaada"

    Yang, anapendekeza kuwa ni vema kama mtandao ukaanzishwa wa kuwasaidia wakina mama ambao watoto wao wamefariki badala ya kusubiri msaada wa serikali.

    "Wakina mama hawa wanaweza kupata msaada kutoka kundi Fulani. Tuko kwenye zama za mtandao wa internet. Nadhani serikali au jumuia zisizo za kiserikali zinaweza kuwa na mitandao au majukwaa kwa ajili ya wakina mama hao kuwasiliana zaidi, na kuratibu shughuli mbalimbali"

    Kutokana na utafiti uliofanywa na Yang, hivi sasa hapa China kuna zaidi ya familia milioni moja ambazo watoto wao wamefariki. Itakapofika mwaka 2035, idadi hiyo itafikia zaidi ya milioni 10.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako