• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping asema China siku zote itajiendeleza kwa amani

    (GMT+08:00) 2013-03-17 19:25:51

    Rais Xi Jinping wa China alipotoa hotuba leo kwenye ufungaji wa mkutano wa kwanza wa bunge la 12 la umma la China alisema, watu wa China wanapenda amani, na China siku zote itafuata njia ya kujiendeleza kwa amani. Rais Xi Jinping amesema, ndugu wa mikoa ya utawala maalumu ya Hong Kong na Macau wanapaswa kutilia mkazo zaidi maslahi ya jumla ya taifa, na ya Hongkong na Macau, na kulinda na kuhimiza kwa pamoja ustawi na utulivu wa muda mrefu wa mikoa hiyo . Ndugu wa Taiwan na wa China bara wanapaswa kushirikiana katika kuunga mkono, kulinda na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa kando mbili za mlango bahari wa Taiwan, kuboresha maisha ya ndugu wa kando mbili na kufanya juhudi kwa pamoja ili kujenga mustakbali mpya wa taifa la China.

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, China ikiwa ni nchi inayoendelea, ingependa kubeba wajibu wa kimataifa inaopaswa, na itashirikiana na nchi mbalimbali duniani katika kulinda amani na ustawi wa dunia nzima katika karne ya 21. Amesisitiza kuwa, kufuata njia ya kujiendeleza kwa amani ni nia thabiti ya China, na kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi yake pia ni nia thabiti ya China. Kanuni hizo mbili zinaweza kutekelezwa bila kukinzana, pia zinalingana na kanuni za kulinda utulivu wa kikanda na amani ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako