• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kwanza wa Bunge la 12 la umma la China wafungwa

    (GMT+08:00) 2013-03-17 19:51:40

    Mkutano wa kwanza wa bunge la 12 la umma la China umefungwa leo hapa Beijing. Rais Xi Jinping wa China alipotoa hotuba kwenye ufungaji wa mkutano huo amesema, "ndoto ya China" kimsingi ni ndoto ya umma, ambayo ni lazima itimizwe kwa kutegemea wananchi, na ni lazima kuleta manufaa kwa wananchi siku hadi siku.

    Rais Xi Jinping amesema, kutimiza ndoto ya China ni lazima kuenzi moyo wa China, yaani moyo wa taifa ambao kiini chake ni uzalendo, na moyo wa kwenda na wakati ambao kiini chake ni kufanya mageuzi na uvumbuzi. Moyo huo ni roho ya kustawisha taifa na kuongeza nguvu ya nchi ambayo inaweza kukusanya nguvu na kushirikisha wananchi wote. Rais Xi amesema, wananchi wa makabila mbalimbali wanapaswa kushikilia na kuenzi moyo wa taifa na kufuata moyo wa kwenda na wakati, kuendelea kuimarisha mshikamano wa taifa na moyo wa kujiendeleza kwa kujitegemea, na daima wawe na ukakamavu na ari kubwa katika njia ya kusonga mbele .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako