Rais wa zamani wa Liberia Moses Blah amefariki jana baada ya kuugua kwa muda mrefu. Marehemu Blah aliyezaliwa tarehe 18 Aprili mwaka 1947, alikuwa rais wa awamu ya 23 wa Liberia kwa miezi miwili mwaka 2003, alithibitishwa kufariki kutokana na ugonjwa wa moyo katika hospitali ya John F. Kennedy huko Monrovia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |