• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0402

    (GMT+08:00) 2013-04-23 14:59:41
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Yohana Marwa Magaigwa wa klabu ya Wanakemogemba S.L.P 71 Tarime Mara-Tanzania anaanza kwa kusema nashukuru sana kwa kunifahamisha kuhusu hiyo ziara ya Rais mpya wa Taifa la China na ninawaahidi kusikiliza vipindi vyote mtakavyorusha hewani. Nawatakia kazi njema katika ujenzi wa CRI idhaa ya kiswahili.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Yohana Marwa Magaigwa kwa barua yako fupi sana, tunatumai kuwa umesikiliza hotuba ya rais mpya wa China Xi Jinping aliyoitoa kwenye ukumbi wa kituo cha kimataifa cha mikutano cha mwalimu Nyerere, ambayo tuliirusha moja kwa moja asante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Mogire Machuki wa Kisii Kenya anasema awali ya yote natoa shukrani zangu za dhati kwa barua yenu fupi kunifahamisha kuwa barua zangu kwenu zimefika na kwa namna moja zinaendelea kusaidia katika kuyaboresha matangazo ya CRI. Asante sana.

    Pili nikiwa mmenitumia zawadi ndogo kwa kushiriki kwenye Hojaji kuhusu mikutano miwili iliofanyika Beijing kwa mafanikio makubwa. Zawadi nikiipokea nitawaarifu na fahamu kwamba zawadi ninazozipokea kutoka CRI japo mnasema ni ndogo ndogo kwangu ni za thamani sana maana zinanipa moyo wa kuendelea kushirikiana na CRI na pia ni kumbukumbu maalum kwangu kumiliki zawadi iliyo na nembo ya CRI. Zawadi mnazonitumia huwa nazihifadhi vizuri sana kwa miaka yote ambayo nimekuwa na urafiki na CRI. Hivyo zawadi kutoka CRI hata kama ni ndogo kiasi gani huwa naithamini sana. Shukrani za dhati huku nikiendelea kufuatiliia hali nzima ya siasa nchini China kupitia vyombo vya kigeni hususani ziara ya hivi punde ya Rais mpya wa China Bw. Xi barani Afrika. Asante sana.

    Nasi tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Mogire Machuki kwa barua yako, pia tunakushukuru kwa kushiriki kwenye hojaji kuhusu mikutano miwili iliyofanyika Beijing kwa mafanikio makubwa, tunathamini sana mchango wako wa mawazo yako, ahsante sana.

    Na sasa ni zamu ya msikilizaji wetu Okong'o Magaigwa wa Kemogemba Club S.L.P 71 Tarime Mara Tanzania naye anaanza kwa kusema hamjambo wote hapo katika studio za idhaa ya kiswahili ya radio China kimataifa ni matumaini yangu kuwa leo kwa mara nyingine najitokeza katika kipindi hiki cha sanduku la barua kuwashukuru na kuwapongeza kwa juhudi mnazozifanya katika matangazo ambayo wengi tunayafurahia na kupata uelewa mpya kwa kuyasikiliza. Radio China inaendelea kupasua mawimbi na kushikilia nafasi za juu katika nyanja hii ya utangazaji kimataifa kwa nchi za nje hivyo ninawaombea mzidi kuchanua siku hadi siku kutokana na jinsi matangazo haya yalivyopangika inavyotakiwa. Nawashukuru tena kwa mara nyingine nikisema Mungu awape nguvu zaidi. asanteni sana.

    Shukran nyingi msikilizaji wetu Okong'o Magaigwa kwa barua yako ya pongezi kuhusu juhudi tunazochukua ili kuhakikisha matangazo yanazidi kuwa mazuri. Timu nzima ya idhaa ya Kiswahili inajitahidi kutumia uzoefu wao na maarifa yao ili kuwaletea matangazo ambayo yatawaridhisha wasikilizaji wa rika lote, ahsante sana.

    Na mwisho tunawaletea ujumbe uliotumwa na wasikilizaji wetu kupitia kwenye tovuti yetu na kwanza ni msikilizaji wetu Salum Mgaya wa Shekilango Dar es salaam baruapepe yake ni salumgaya03@yahoo.com anasema hii ni fursa nzuri kwa watanzania kuboresha mahusiano na China katika nyanja za kiuchumi. Tunaomba Rais Xi Jinping wa China aweke wazi kuhusu ubora wa bidhaa zake zinazoingia nchini Tanzania kwani bidhaa kutoka nchini kwake tunazipenda lakini hazidumu tofauti na bidhaa za nchi nyingine.

    Naye Olais Raphael mwenye baruapepe olais_raphael@hotmail.com anasema napenda sana kusikiliza radio china. Habari nzuri. Napenda rais wa china akija Tanzania asisahau kuhamasisha ujamaa kwa vijana wa Tanzania na Afrika. Napenda ashirikiane nasi. Atafute mtu wa karibu kuratibu ushirikiano huo kwani dunia ya sasa ukijulikana wewe mjamaa dunia inakutenga.

    Msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba baruapepe ni epst01@hotmail.com anasema pongezi za kipekee ziwaendee watangazaji mama Chen na Fadhili waliotuletea kwa uzuri na umakini mkubwa hotuba ya rais mpya wa China Xi Jinping aliyetembelea Tanzania.

    Na mwisho ni ujumbe kutoka kwa msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba mwenye baruapepe epst01@hotmail.com anasema napongeza hotuba ya rais Xi Jinping aliyoitoa leo nchini Tanzania katika kituo cha mwalimu nyerere ikiwa ni ziara yake ya kwanza kabisa nchini Tanzania, hotuba hiyo imeonyesha wazi kuwa nchi ya China na Tanzania zimejenga urafiki wa muda mrefu ambao umeleta mahusiano mazuri sana katika sekta mbalimbali kwa mfano sekta ya uchumi inaonekana kukua kwa kiwango kikubwa sana katika bara la Afrika, rais Xi amebainisha kuwa vitega uchumi vilivyowekezwa barani Afrika vimezidi dola za kimarekani bilioni 15, hii inaonesha wazi kuwa China iko mstari wa mbele katika kuinua uchumi kwa nchi za afrika. Mimi binafsi nafurahia sana kuona uhusiano kati ya China na Afrika unadumu zaidi na zaidi.

    Tunawashukuru kwa dhati wasikilizaji wetu wote mliotutumia maoni kupitia tovuti yetu, pia tunawashukuru wasikilizaji wetu wote waliosikiliza hotuba ya rais mpya wa China Xi Jinping aliyoitoa kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere, ambayo mimi na Fadhili tulijaribu kuwaelezea kilichozungumzwa kwenye hotuba hiyo. Mwisho tunawaomba muendelee kusikiliza matangazo yetu na kutuandikia maoni namapendekezo yenu, ahsante sana.

    Tarehe 25 Rais Mpya Xi Jinping alitoa hotuba isemayo: Tuwe marafiki wa kutegemeka na wenzi wa dhati daima kwenye Kituo cha Kimataifa cha mikutano cha Mwalimu Nyerere, katika hotuba yake isemayo amezungumza masuala mengi kuhusu kuendeleza uhuriano wa kirafiki na ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Tanzania na China na Afrika. Na amesisitiza kuwa, Msingi na mizizi ya uhusiano kati ya China na Afrika iko kwa wananchi wa pande mbili. Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya marafiki wa Afrika wamekuwa nyota maarufu kwenye jukwaa la michezo nchini China. Na tamthiliya ya China ya "Doudou na mama wakwe zake" inayooneshwa nchini Tanzania imewafanya watazamaji wa Tanzania wajihisi ladha za aina mbalimbali za maisha ya familia za raia wa China.

    Sasa tunawaletea ufupi wa ripoti hiyo. Karibuni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako