• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0416

    (GMT+08:00) 2013-04-23 15:00:16
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Stephen Magoye Kumalija wa S.L.P 1067 Kahama Shinyanga Tanzania, anaanza kwa kusema kwanza pokeeni salamu zangu nyingi za mwaka mpya wa 2013 kutoka hapa Kahama, bila shaka mnaendelea vyema na shughuli zenu mbalimbali za kila siku na kutuletea matangazo muhimu kutoka sehemu na maeneo mbalimbali hapa Ulimwenguni.

    Sasa nachukua fursa hii kuwapongeza wafanyakazi wote wa idhaa ya Kiswahili ya redio China kimataifa, ambapo wafanyakazi karibu wote wa idhaa ya Kiswahili walitumia fursa ya kutuma salamu zao za kututakia heri ya mwaka huu wa 2013. Sitahau kuwapongeza viongzi wa China akiwemo rais mpya Xi Jinping. Pia napenda kuwapongeza kwa kipindi cha China Machoni Mwetu kinachoendeshwa na watangazaji wazuri wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI Bw. Fadhili Mpunji na Bi Pili Mwinyi ambapo kipindi cha tarehe 3 Januari kilinigusa sana kwani kilikuwa kinahusu wageni mbalimbali wanaotembelea China, jinsi wanavyotatizwa na lugha ya kichina.

    Kweli lugha ya kichina ni ngumu sana, hata mimi nilipopata fursa ya kutembelea China, miaka miwili iliyopita lugha ya kichina ilikuwa inanitatiza sana nilipotaka kuwasiliana na marafiki wachina wakati wa kununua vitu madukani. Lakini nashukuru wachina ambao ni wafanyakazi wa idhaa ya Kiswahili pamoja na waafrika wenzangu ambao wamekuwa wenyeji wameifahamu na kuielewa lugha hiyo. Walinisaidia sana katika upande wa mawasiliano. Hivyo sina budi kuwapongeza watangazaji wa kipindi hicho na naomba kiendeleee kwani kinatuelimisha mambo mengi kuhusu China. Mwisho nawatakia mafanikio mema.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Stephen Magoye Kumalija kwa barua yako, pia kwa niaba ya wafanyakazi wote wa CRI napokea pongezi zako kwa mikono miwili. Kuhusu kipindi cha China machoni mwetu, kwa kweli kama ulivyosema kinaelimisha sana watu wa Afrika kwani China ina mambo mengi sana ambayo hayatambulikani ulimwenguni, ndio maana tuliamua kuanzisha kipindi hicho ili kuwafahamisha mambo mbalimbali yanayotokea hapa China, tunashukuru kwamba mmekikubali na kukipenda, ahsante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba baruapepe yake ni epst01@hotmail.com anasema Awali ya yote naendelea kuwapongeza sana idhaa ya kiswahili ya redio China kimataifa kwa kuweza kutujuza mambo kemkem, hata tukio la hivi karibuni la kuporomoka kwa jengo lenye ghorofa kumi na sita nchini Tanzania katika jiji la Dar es salaam, kweli ni simanzi kubwa watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha, mimi binafsi nawapa pole nakuwaombea kwa mungu majeruhi wote wapone haraka, pia pongezi nyingi kwa vikosi mbalimbali vya uokoaji vinavyo endelea kujitolea hata marafiki zetu wa China kujitolea kwa dhati na kufika katika eneo hilo kweli ni ishara nzuri ya umoja na mshikamano wa dhati kati ya China na Tanzania, endeleeni na moyo huo huo.

    Naweza nikaelezea tajiriba yangu kuhusu ziara ya rais Xi Jinping wa jamuhuri ya watu wa China kwa kutembelea nchi za Afrika, ni habari zilizo wazi kabisa kuwa rais huyo ni mfano wa kuigwa na marais wengine kutoka nchi nyingine zilizoendelea kiuchumi, tathmini yangu binafsi kuhusiana na ziara hiyo kwa nchi za Afrika, kimsingi ziara hiyo imefungua ukurasa mpya kabisa kati ya China na Afrika ikiwa ni ziara yake ya kwanza kabisa tangu ashike madaraka ya kuliongoza taifa hilo kubwa la China lenye uwezo wa kiuchumi. Mengi ameweza kuyafanya katika baadhi ya nchi za Afrika kwa kutiliana saini mikataba yenye lengo la kuzisaidia nchi za Afrika, kweli nimependezwa sana na jambo hilo.

    Nasi tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba kwa barua yako, kwanza tunapenda kuwapa pole watu wote waliokumbwa na mkasa huo, na kutoa salamu za rambirambi kwa wafiwa. Kwa kweli ni ajali mbaya sana, Mungu atawapa moyo wa subira. Kuhusu ziara ya rais mpya China Xi Jinping hata sisi wachina pia tumefurahia kwa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kuitembelea katika Afrika kwani ni rafiki yetu mkubwa tangu enzi na dahari. Ahsante sana.

    Sasa tunawaletea ujumbe tuliotumiwa na wasikilizaji wetu kupitia kwenye tovuti yetu, msikilizaji wetu wa kwanza ni Ras Manko Ngogo S.L.P 71, Tarime, Tanzania anasema nawapa mkono wa heri na pongezi kwa matangazo ya CRI, hususani muda wote wa ziara ya rais Xi Jinping nchini Tanzania. Hakika mnaonyesha jinsi mlivyotilia mkazo wa kutuletea matangazo kila saa. Hongera CRI.

    Naye Mihotho Daniel baruapepe yake ni danielmihoto@yahoo.co.za anasema nafurahia huu ushirikiano wa China na Afrika kama ingewezekana nchi zote za Afrika zijiunge na wachaina waache kuwategemeya wamerekani na wafaransa ambao mpango wao mkubwa ni kuwaunga mkono mashoga (gays) katika luga ya kingereza na kuleta vita katika Afrika na Mungu awabariki wachina na haya mawazo yao.

    Ujumbe wa mwisho unatoka kwa msikilizaji wetu Mcharo Mshana mwenye baruapepe mcharo_mshana@yahoo.com anasema ushirikiano wa China na Tanzania niwa jadi, China ni rafiki mkubwa wa Tanzania na imejikita zaidi Barani Afrika kwani ni eneo muhimu la kibiashara na upatikanaji wa malighafi bora zaidi. Barani Afrika unaweza kuchukua bidhaa ukaongeza thamani. naamini China ni bora Barani Afika kuliko ulaya. Tahadhari kubwa ni uuzaji wa silaha nisingependa kuona shehena za silaha kutoka China zikiingizwa Afrika. Karibu China kwa Amani.

    Tunawashukuru sana wasikilizaji wetu wote mnaotupata kwenye tovuti yetu, tunawaomba muendele kusoma matangazo yetu na kusikiliza idhaa ya Kiswahili ya redio China kimatafa na bila kusahau kutuandikia maoni na mapendekezo yenu, ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako