• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. Li Keqiang azitaka Israel na Palestina ziweke mazingira mazuri ya kuanzisha tena mazungumzo ya amani

    (GMT+08:00) 2013-05-08 21:30:19

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo hapa Beijing amesema, China inazitaka Israel na Palestina zichukue hatua halisi ili kuondoa vizuizi, na kuweka mazingira mazuri ya kuanzisha tena mazungumzo ya amani yatakayopata maendeleo ya halisi.

    Bw. Li Keqiang amesema hayo leo alasiri alipokutana na waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu ambaye yuko ziarani nchini China. Viongozi hao pia wameshiriki kwenye hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kweye sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, teknolojia, na elimu. Li Keqiang amesema, suala la Palestina ni suala kuu linaloathiri amani na utulivu ya sehemu ya Mashariki ya Kati, na mazungumzo ni njia sahihi ya pekee ya utatuzi wa suala hilo.

    Netanyahu amesema, Israel inapenda kusukuma mbele ushirikiano katika uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, kubana matumizi ya maji, kilimo, ufugaji na nishati endelevu, kuhimiza maendeleo ya pamoja ya nchi hizo mbili, na kuboresha maisha ya watu wao. Israel inafurahia mchango wa China katika mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati.

    Li Keqiang na Netanyahu wamekubaliana kuwa idara husika za pande zote mbili zitaunda vikundi kazi maalum, kutafiti njia ya kufanya ushirikiano katika mambo ya uchumi na jamii, na kutunga na kutekeleza mpango wa ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako