• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanajeshi wa Misri waliotekwa nyara kwenye eneo la Sinai waachiliwa huru

    (GMT+08:00) 2013-05-22 17:53:02

    Kundi la Jihad katika Peninsula ya Sinai, nchini Misri limewaachia huru wanajeshi saba waliowateka nyara wiki iliyopita.

    Msemaji wa jeshi la Misri amesema, wanajeshi hao wanaelekea Cairo baada ya kuachiwa huru kufuatia juhudi za upelelezi zilizofanywa na jeshi la Misri likishirikiana na wakuu wa makabila na familia za Sinai.

    Alhamisi iliyopita, kundi la wapiganaji liliwateka nyara wanajeshi na polisi saba katika eneo la Green Valley la Sinai Kaskazini, kilomita 20 kutoka mji mkuu wa jimbo la Arish. Wapiganaji hao walikuwa wakidai kuachiwa huru kwa ndugu zao waliofungwa katika gereza la Tora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako