• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0521

    (GMT+08:00) 2013-06-03 15:47:53
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Mchana J Mchana wa Chuo Kikuu cha Jordan Morogoro Tanzania, anaanza kwa kusema awali ya yote napenda kuwapa salamu zangu nyote hapo radio China kimataifa, pia msisikitike kwa ukimya wangu. Hii ni kwa upande wa mawasiliano. Lakini kwa usikilizaji nipo nanyi kila siku, leo pia nampa hai balozi wa Tanzania hapo China vipindi vyote alipohojiwa nimevisikia.

    Ni sawa ni balozi wa nchi lakini naye awe mtetezi wa mkoa wake wa manyara kwani pale mkoani pana miradi mingi, nani wakulima wazuri sana wa mazao kama mahindi, maharagwe, mbaazi, mpunga, ngano, vitunguu vya aina zote. namuomba atusaidie kutupatia wataalamu, kwani naamini China hawana uchoyo cha kutoa utaalamu, pia kupitia kwenu naomba mumpatie ujumbe huu. Ili sehemu kama, Galapo, Magugu, Dareda, Kateshi, Endasaki, wafaidike na ubalozi wake, mimi ni mkazi wa Galapo Morogoro ni kikazi tu, ahsanteni sana.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Mchana J Mchana kwa barua yako fupi. Ni kweli muda mrefu umepita hatujaweza kuwasiliana nawe, lakini tunajua ni kutokana na kubanwa na shughuli nyingi, halafu kuhusu kumfikishia ujumbe Balozi tutajitahidi ahsante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba baruapepe yake ni epafra stanley epst01@hotmail.com anasema kwa kweli serikali ya China inahitaji kupewa pongezi za dhati kwa juhudi kubwa ilizozionesha kwa raia wake wa wilaya ya lushan mkoa wa Sichuan baada ya kukumbwa na tetemeko la ardhi hivi karibuni. Jambo lililonifurahisha mimi binafsi ni serikali ya China kukamilisha utandazaji wa mabomba ya maji katika eneo hilo kwa asilimia 99.36. jamani ni jambo linalofurahisha sana na kuleta faraja kwa wakazi wa eneo hilo la lushan. Na hapa nimeandika shairi la lenye beti mbili kwa ajili ya kuipongeza serikali ya China.

    Pongezi zangu natoa, kwa nahodha makini,

    Chombo kukiongoza, kwa dhati kushuhudia,

    Agizo kulitoa, nalo kutekelezwa,

    Faraja kuiona, kwa nahodha wao makini.

    Waweza jiuliza, nahodha huyo ni nani?

    Hebu ngoja nikueleze, ni katibu mkuu yakini

    wa chama cha kikomunisti, ambaye pia ni rais

    wa China yetu makini, si mwingine ni Bw. Xi jinping

    Kiongozi huyu ameonesha kuwa serikali ya watu wa China iko mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Sichuan na kuleta maafa makubwa wanahitaji kupewa kipaumbele kwa kuendelea kuwasaidia kwa kutoa huduma mbalimbali za kijamii. Kimsingi rais Xi na serikali yake ni mfano mkubwa wa kuigwa na mataifa mengine kote ulimwenguni, kwani wameweza kuonesha uwajibikaji mkubwa kwa kutoa huduma za msingi katika wilaya ya lushan mkoani Sichuan baada ya kukumbwa na tetemeko la ardhi. Ninaendelea kuitakia kila la heri na utendaji kazi mwema serikali ya China chini ya uongozi wake rais Xi jinping.

    Shukran za dhati msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba kwa barua yako murua kabisa ambayo ndani yake umetuandikia shairi ingawa lina beti mbili lakini ni zuri sana. Kuhusu tetemeko la ardhi lililotokea huko Sichuan kwa kweli hivi sasa hali imeboreshwa kwa kiasi kikubwa huko kwani waathirika wote wamepatiwa huduma zote muhimu, ahsante sana.

    Msikilizaji wetu Lameck Nzingo wa S.L.P 71 Kigoma Tanzania anasema barua yake inahusiana na Tamthiliya ya Kichina ya Doudou na Mama Wakwe Zake. Kusema kweli ninaipenda sana hii tamthilia yaani naipenda sana kupita maelezo lakini tatizo ni jinsi inavyoisha hivi inaisha kama ilivyoisha au TBC1 wameikatisha? tafadhali naombeni jibu moyo wangu upate kutulia. Pili ninaweza kuipata kwenye dvd kama naweza kuipata tafadhalini ninaomba kuelekezwa namna ya kipata, mwisho nawapongeza wote waliohusika kufanikisha tamthilia hii bila kusahau kutoa shukrani zangu za dhati kwa wahusika wote waliocheza tamthilia hii hasa mao Doudou, Yu Wei, mrembo Yu hao na Panmeili bila kumsahau mama wa visa Yang shine ametisha mbayaaaaa.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Lameck Nzingo kwa barua yako kweli umetufurahisha sana uliposema wanatisha mbaya, kwani ni kweli kwasababu ni tamthilia nzuri sana, tunataraji kuwa tutakapoonesha tamthilia nyingine pia mtaipenda zaidi, ahsante sana.

    Mwisho yunawaletea ujumbe tuliotumiwa na wasikilizaji wetu kwenye tovuti yetu, na kwanza ni Kiyonga Daniel Esekon baruapepe yake ni kiyongadanielesekon@gmail.com anasema nafurahia CRI kwa matangazo maalum na watangazaji wote. dj Mos ni kaa la moto na Jacob Mogoa sauti ya simba.

    Ujumbe mwingine unatoka kwa msikilizaji wetu Ramadhan Mchome wa S.L.P 5 Ngorongoro Tanzania anasema naipenda idhaa ya kiswahili ya redio China, kweli nimefurahishwa na ujio wa rais wa China Tanzania, kwani inatuonesha jinsi gan tuna upendo na nchi nyingine. kila la heri nchi hizi mbili katika ushirikiano ahsante.

    Ujumbe wa mwisho unatoka kwa Mogire Machuki baruapepe yake ni oscarmogire@yahoo.com anasema ujumbe wake ni kuhusu "Sauti ya Bahari ya Kusini" kweli CRI ina mikakati ya kuhakakisha kuwa raia wake wanapata taarifa za uhakika kuhusu taifa lake na uhusiano na mataifa ya kigeni.

    Tunawashukuru sana wasikilizaji wetu wote mliotutumia ujumbe kupitia kwenye tovuti yetu, tunaomba muendelee kusikiliza matangazo yetu na kutupa maoni na mapendekezo, ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako