• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0604

    (GMT+08:00) 2013-06-03 15:49:10
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba mwenye baruapepe epst01@hotmail.com. Anaanza kwa kusema kwanza kabisa pokeeni, pongezi nyingi nchi ya China kwa kuweza kushika nafasi ya tisa duniani kwa kuwekeza miradi 152 barani Afrika, mimi binafsi ninaweza kusema kuwa nchi ya China imekuwa mstari wa mbele kujenga uhusiano ulio mzuri na nchi za Afrika ikiwa na lengo la kuzisaidia nchi hizo.

    Nikitoa mfano kwa nchi yetu ya Tanzania ambayo ni rafiki mkubwa wa China kwa miaka mingi, kwa kweli nchi yetu inaendelea kunufaika katika sekta mbalimbali, kwa mfano sekta ya miundo mbinu ikiwemo ujenzi wa barabara na majengo, yote hayo yameweza kufanywa na makampuni kutoka China, hatimaye leo hii tunaweza kusafiri kwa raha mustarehe kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine na kitu kingine kizuri ni uingizaji wa pikipiki kutoka china, nazo kwa kiwango kikubwa zimesaidia kurahisisha usafiri katika maeneo ambayo ni vigumu kuyafika. Mimi ninaendelea kuipongeza nchi ya China kwa kushika nafasi ya 9 duniani kwa kuwekeza miradi mingi barani Afrika.

    Mbali na hayo pia ningependa kuyapongeza maonesho ya kimataifa ya bustani nchini China. Ikiwa ni maonesho ya 9 ya kimataifa ya mabustani nchini china ambayo yamefunguliwa Beijing ni matumaini yangu kuwa maonesho hayo yatajumuisha watu wengi sana na yatakuwa na yenye mvuto wa aina yake, ninaendelea kuwapongeza na kuwashukuru sana CRI kwa kutuhabarisha juu ya maonesho hayo kwa njia ya tovuti ya CRI, asanteni sana, tena endeleeni kutufahamisha mengi zaidi, mimi msikilizaji wenu furaha yangu ni kusikiliza matangazao yenu kwa njia ya redio na pia kufuatilia tovuti yenu ambayo husheheni mambo mengi yenye manufaa makubwa kwangu.

    Shukran za dhati msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba kwa barua yako, kwa kweli China inajitahidi kushirikiana na nchi mbalimbali hususan za Afrika kwani pande hizi mbili ni marafiki wakubwa, na ndio maana inaona ni vyema kuwekeza Afriika kwasababu waswahili wanasema sadaka huanzia nyumbani, na China kwa Afrika ni kama nyumbani. Mwisho piua tunakushukuru kwa kusikiliza vipindi vyetu kuhusu maonesho ya mabustani ya hapa China, ahsante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Juma N. Katala wa S.L.P 452 Bongomela Ndala Tabora Tanzania anasema salamu kwa watangazaji wa redio China Kimataifa na hongera sana kwa kazi zenu nzuri za kila siku za kutuhabarisha taarifa mbalimbali. Mimi ni mzima wa afya njema na ninaendelea kusikiliza redioChinakila siku kupitia KBC.

    Nilifarijika sana na kipindi cha tarehe 19.3.2013 ambacho mlimhoji na kumuelezea mama mmoja wa Kenya aliyekuwa na watoto zaidi ya 20 anaowatunza. Nilivutiwa sana kwa wema na ukarimu na moyo wa mzuri wa imani kwa mama huyo. Maombi yangu ni kuwa mashirika, taasisi na watu binafsi wamsaidie misaada ya hali na mali, ninimani watoto wale wanazidi kukua na wanazidi kuongezeka kwa hiyo mahitaji yao nayo yanazidi kuongezeka.

    Pia ushauri wangu kwa mama huyo ajitahidi kumpata mtu au watu wengine wa kumsaidia endapo tu hatujui ni lini mtu anaweza kufariki. Ila tunamuombea maisha marefu yenye afya njema, lakini umri nao utakuwa kikwazo kwa kuwahudumia watoto hao kama alivyo sasa. Hongereni sana kwa tafiti zenu hizo mbalimbali.

    Shukran za dhati msikilizaji wetu Juma N. Katala kwa barua yako, ambayo inaonesha unafuatilia kwa karibu sana vipindi vyetu, tunakupongeza kwa hili. Lakini pia nasi tunampongeza mama huyo kwa moyo wa ujasiri wa kuwakusanya watoto wenye mahitaji na kuamua kuwatunza, kwa kweli hiyo ni hatua nzuri aliyoifikia mama huyo, wahenga wanasemna kutoa ni moyo usambe utajiri. Ahsante sana.

    Mwisho tunawasomea ujumbe tuliotumiwa na wasikilizaji wetu kwenye mtandao, na kwanza ni ujumbe kutoka kwa Elie Ndiho baruapepe yake ni ndihoelie06@gmail.com anasema Dajia hao! Salamu zangu ziwafikie wasikilizaji wote wa hapa mjini Bujumbura. Nawatakia maisha mema na wajae neema kutoka kwake Mungu. Xiexie da jia

    Ujumbe mwingine ni kutoka kwa Mogire Machuki baruapepe ni oscarmogire@yahoo.com naye anasema kutoka Kisii Kenya naitakia CRI kila la kheri kwa kuendelea kufikia ndoto yake ya kuifahamisha dunia kuhusu taifa la China. Leo hii kumefunguliwa kituo cha 90 cha FM cha CRI hongera sana. Msikilizaji wetu Philemon baruapepe yake ni philemonsamwel@ymail.com anasema naomba zitolewe nakala za tamthilia hii ya Doudou na wakwe zake kwani hainiishi hamu.

    Naye Etienne wa baruapepe etienbmpiga@yahoo.fr anasema Naipenda CRI sana kipindi cha cheche zetu; Mungu awabariki nyote

    Yakubu anasema Ninayo furaha kuona lugha ya Kiswahili inazungumzwa kote. lakini Afrika Kusini bado iko nyuma.

    Msikilizaji wetu Haidara baruapepe haidallahh@yahoo.fr anasema Hongera sana kwa wandishi ha habari wa CRI. Pili Mwinyi endelea kufanya vizuri, Burundi tunakusikia. Lakini kero yetu ni kwamba hakuna taarifa yoyote kutoka Burundi wakati uchina ni mshirika mkubwa wa maendeleo ya Burundi. Wiki iliopita kiongozi wa CRI akishirikiana na balozi ya uchina nchini Burundi Yu xuzhong walizinduwa rasmi matangazo ya CRI nchini Burundi katika hafla, serikali ya Burundi iliwakilishwa na waziri wa vijana na utamaduni.

    Mwisho ni ujumbe kutoka kwa Abdallah abdallahrashid48@yahoo.com Ahsante kwa msaada wenu adhimu wa kuwasaidia watu maarifa, kuadabisha, pamoja na mengineo.

    Tunawashukuru wasikilizaji wetu wote mnaotupata kwenye mtandao, tunawaomba muendelee pia kusikiliza matangazo yetu ya redioni na kutoa maoni na mapendekezo yenu, ahsanteni sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako