• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua 0611

    (GMT+08:00) 2013-06-11 09:25:59
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba wa baruapepe epst01@hotmail.com anaanza kwa kusema ninaendelea kuwaunga mkono marafiki zangu wapendwa wa idhaa ya kiswahili redio China kimataifa kwa kuendelea kutujuza kwa uzuri habari kemkem na zenye mvuto wa kipekee kwetu sisi wasikilizaji wenu. Ikiwa ni mei 18 ambayo ni siku ya 37 ya kimataifa ya majumba ya makumbusho yenye kaulimbiu "jumba la makumbusho (kumbukumbu na uvumbuzi) mabadiliko ya kijamii".

    Kwa kweli majumba hayo ya makumbusho yamekuwa msaada mkubwa kwa kizazi cha leo na hata kizazi kijacho kwani kitajifunza asili ya binadamu na maendeleo yake katika utengenezaji wa zana, vile vile majumba hayo yamekuwa ni kivutio kikubwa kwa watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani, na kukuza uchumi kwa nchi husika. Kwa ujumla ninawapongeza sana CRI kwa kutujuza habari mbalimbali zilizo murua kabisa juu ya maadhimisho hayo ya majumba ya makumbusho yanayofanyika Afrika.

    Pia anasema "Kongamano kuhusu Afrika la Baraza la uchumi la dunia limemalizika kwa kutoa wito wa kuwekeza zaidi katika Afrika" napenda kutoa pongezi nyingi kwa nchi ya Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa kongamano la 23 kuhusu Afrika la Baraza la Uchumi na Dunia (WEF) lililo fanyika nchini humo kwa muda wa siku tatu. Katika tathimini yangu, mimi binafsi ninaona kuwa kongamano hilo limeleta sura nzuri yenye matumaini kwa nchi nyingi za Afrika, jambo lililonifurahisha ni kauli mbiu iliyojumuisha mambo matatu, kwanza ni kuongeza kasi ya upanuzi wa uchumi, pili ni kusukuma mbele mikakati ya miundo mbinu na tatu ni kutumia maliasili za Afrika. Kimsingi mambo hayo iwapo yatatekelezwa kikamilifu nimatumaini yangu kuwa bara la afrika litapiga hatua kubwa kimaendeleo. Mwisho nawashukuru sana CRI kutujuza juu ya mkutano huo kupitia tovuti ya yenu iliyosheheni habari lukuki kutoka pande nne za dunia.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba ambapo leo hii umezungumzia mambo mawili ambayo yote ni muhimu kwanza ni kuhusu siku ya 37 ya kimataifa ya majumba ya makumbusho na pia kuhusu Kongamano la Baraza la uchumi la dunia lililojadili kuhusu Afrika. Hata sisi pia tunalipongeza kongamano hilo kwani lilikuwa na lengo la kupanua na kukuza uchumi wa Afrika ahsante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Philp Ng'ang'a Kiarie wa S.L.P 601 Maragua Kenya anasema salamu zangu ziwafikie watangazaji wote pamoja na wasimamizi wa idhaa ya Kiswahili ya Redio China Kimataifa. Pia pongezi ziwafikie wasikilizaji wote walioshinda nafasi mbalimbali na walioshiriki kwenye shindano la chemsha bongo la miaka 45 tangu China na Tanzania zianzishe uhusiano wa kibalozi. Ni furaha kuwa hata watanzania wanapenda kusikiliza vipindi na matangazo ya idhaa ya kiswahiliya CRI.

    Ukweli ni kwamba redio hii inatufurahisha sana sisi wasikilizaji tunaoandika barua kwa vile hamna ubaguzi wa kusoma barua zetu na pia mnazihifadhi na kuziweka hata kwenye matangazo na vipindi vya kwenye tovuti. Kuhusu zawadi za washindi wa nafasi mbalimbali kwenye shindano la chemsha bongo, ni wazi kuwa umewadia wakati ambapo idhaa ya Kiswahili imedhihirisha kuwa uhusiano kati yake na wasikilizaji wake ni wa kunufaishana, kwa mfano wasikilizaji walioshinda cherahani wamepata fursa nzuri ya kuanzisha biashara ndogo ndogo na kuanza kupata mapato ili kukabiliana na wakati huu mgumu, ambapo gharama ya maisha inaendelea kupoanda. Nashukuru sana.

    Nasi tunakushukuru sana msikilziaji wetu Philp Ng'ang'a Kiarie kwa kuendelea kusikiliza matangazo na vipindi vyetu. Redio China China Kimataifa inajali sana wasikilizaji wake na ndio maana huwa inajaribu kutafuta kila njia za kuweza kuwasaidia wasikilizaji wetu hususan kupitia mashindano ya chemsha bongo na kutoa zawadi mbalimbali, ahsante sana.

    Mwisho tunawaletea ujumbe kutoka kwa wasikilizaji wetu wanaotembelea tovuti yetu na kwanza ni kuoka kwa Janneth baruapepe ni jenituu@yahoo.com anasema Kiswahili sasa kimeenea sana, maoni yangu ni sisi wazawa wa lugha tupewe nafasi ya kukiendeleza huko nje ili kipate mashiko Duniani.

    Msikilizaji wetu ANN anasema mimi ni mpishi wa Kenya, nafanya kazi katika kampuni moja ya wachina, nataka kuwapikia matajiri wangu vitoweo vya kichina ili kuwafurahisha zaidi. zamani nimesoma upishi wa kichina kwenye mtandao huo wa Kiswahili, lakini leo nimeshindwa kuupata. Tafadhali niambie kwa namna gani naweza kusoma tena.

    Siraji shemaua wa S.L.P 18 Korogwe Mgila Tanzania anasema Hongera radio ya China kwa kukikuza kiswahili mungu awabariki nyote.

    Tunawashukuru kwa dhati wasikilizaji wetu wote mnaotembelea tovuti yetu, na kwa kumjibu msikilizaji wetu ANN ambaye ni mpishi wa Kenya, ni kwamba hivi sasa programu ile kuhusu mapishi ya kichina hatuitangazi, kwani kila baada ya kipindi Fulani huwa tunafanyia mabadiliko vipindi vyetu, tunaomba utuwie radhi kwa hilo. Pia tunawasihi wasikilizaji wetu wote muendelee kusikiliza matangazo yetu na kututumia maoni na mapendekezo yenu, ahsanteni sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako