• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua 0618

    (GMT+08:00) 2013-06-26 16:56:42
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Abdi Saidi Iyulu wa S.L.P 6 Kondoa Tanzania anaanza kwa kusema nampongeza rais wa China kwa msimamo wake wa kutobabaika katika uendeshaji wa siasa ya ujamaa ulioimarika duniani na kuwa kama mfano wa kuigwa na mataifa mengine. Likiwa ni taifa lililojengeka na kufikia hatua ya kuyasaidia mataifa mengine ambayo ni makubwa na madogo. Mfano huu pekee unatosha kuyasuta mataifa ya kibepari yanayolazimisha kuwa mfumo pekee unaofaa ni wa kibepari.

    Suala hili la watu wa mataifa mbalimbali kuelekeza mawazo katika pesa na utajiri mwingineo linatokana na mfumo wa kimataifa wa kipebari, kama njia pekee iliyozoelewa na watu ya daraja la juu kabisa ya kuweza kututawala, kiukoloni na kiukoloni mambo leo. Lakini sio kweli kabisa kwamba suala hili la matumizi ya pesa ndio peke linaloweza kuleta maendeleo katika mataifa yetu. Huu sio wakati wa kung'ang'ani dhana potofu kwasababu ya eti tumezoea tu, wakati hali hiyo inapingana na misingi ya uthamini wa utu.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Abdi Saidi Iyulu kwa barua yako, kwa kweli kama ulivyosema China inajitahidi kufuata sera zake pamoja na mfumo wake wa ujamaa wenye umaalum wa China, pia inajitahidi kuwasaidia wengine pale wanapokumbwa na matatizo bila kutoa masharti yoyote , ahsante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba baruapepe yake ni epst01@hotmail.com anasema matangazo ya Jumatano iliyopita nimeyapata kwa uzuri sana ambapo nimeweza kusikiliza kipindi cha uchumi kilicho angazia mambo ya uchumi, ambapo kuliweza kufanyika mahojiano mazuri na mfanyabiashara kutoka nchini Tanzania akielezea tajiriba yake ya ufanyaji biashara nchini humo.

    Pia kuhusu kipindi cha China Machoni Mwetu nilikipata kwa uzuri sana, kwani uandaaji wa kipindi ulikuwa mzuri, na uliangazia kwa uzuri majira ya joto nchini China. Na watangazaji kutoa tajiriba zao kuhusiana na hali hiyo. Pongezi nyingi kwenu watangazaji Wote wa CRI kwa uandaaji mzuri wa vipindi. Marafiki zangu niwapendao wa idhaa ya Kiswahili redio China kimataifa. Kwa kweli nina furahia sana matangazo yenu na mpangilio mzima wa vipindi vyenu. Mimi ninawatakia kila la heri katika utendaji wenu wa kazi. Udumu urafiki kati yetu.

    Kwanza tunakushukuru sana msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba kwa barua yako, tunakupongeza sana kwani wewe ni msikilizaji ambaye unasikiliza sana matangazo yetu na kutuunga mkono sana. Idhaa ya Kiswahili ya redio China Kimataifa inajitahidi kuwaletea vipindi mbalimbali ambavyo tunaamini kuwa vinawavutia sana, tutaendelea kujitahidi ili kuhakikisha tunamridhisha kila msikilizaji, ahsante sana.

    Na mwisho tunawasomea ujumbe uliotumwa na wasikilizaji kupitia kwenye tovuti yetu na kwanza ni msikilizaji wetu Choma wa Choma au Kamanda wa mashambulizi ya salamu S.L.P 108 Mwamkulu Mpanda mkoni Katavi Tanzania. anasema katika kipindi cha leo, kwanza salamu zenu watagazaji. Na wasikilizaji pamoja na wachambuzi wa vipindi vya matangazo mbalimbali, kuanzia salamu na cheche zetu, jifunze kichina. Mimi nimejifunza mengi sana kupitia radio China. Kwa vipindi vyenu sitawasahau Pili Mwinyi na Fundi Bengo, Moses. Na mkurugenzi wa radio China kimataifa, maana mnaelimisha watu kwa makini na uhakika. Ahsanteni sana Mungu awabariki.

    Ujumbe mwingine unatoka kwa msikilizaji wetu Mogire Machuki baruapepe yake ni oscarmogire@yahoo.com anasema ujumbe kuhusu "China yapenda kushirikiana kwa karibu na serikali ya Kenya " Salamu kutoka kisii Kenya. Hii ni habari njema kwa Wakenya. China ni rafiki wa dhati wa Kenya na nina imani kuwa urafiki huu ni wa kudumu. Ushirikiano baina ya mataifa haya mawili ni wa kuaminika na wa kunufaishana. Asante kwa China kuitambua serikali mpya ya Kenya.

    Naye Siraji Shemaua wa S.L.P 18 Korogwe Mgila Tanzania anasema Hongera radio China kwa kukikuza kiswahili Mungu awabariki nyote

    Mwisho ni msikilizaji wetu Edward Kabamba wa S.L.P 9060 Haydom Manyara Tanzania, anasema CRI kwanini katika kipindi chenu cha salaam msifanye namna yoyote ya kujiunga na radio zilizoko Tanzania tunawapata kupitia masafa mafupi wakati mwingi tunawakosa. Ni mawazo yangu na maoni yangu kwa sababu wanasalam ni wengi sana lakini wachache ndio waelewa.

    Tunawashukuru wasikilizaji wetu wote mnaosoma matangazo yetu kwenye mtandao, tunawaomba muendelee pia kusikiliza matangazo yetu ya redioni na kutoa maoni na mapendekezo yenu, ahsanteni sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako