• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi'an--Mji wenye vivutio maalumu vya historia na utamaduni

    (GMT+08:00) 2013-06-24 09:17:18

    Mali za urithi za utamaduni ni mlango wa binadamu kufahamu historia, na pia ni kumbukumbu ya hadithi za maisha ya binadamu na maendeleo ya jamii. Mji wa Xi'an mkoani Shaanxi ulioko katikati mwa China una historia ya miaka zaidi ya 3,000, na una mali nyingi za urithi za utamaduni. Katika kipindi cha leo, tunakuongoza kutembelea mji huo wenye vivutio maalumu vya historia na utamaduni.

    Wapendwa wasikilizaji, mnaosikia ni muziki unaopigwa na mwanamuziki kwa ala ya Xun. Xun ni ala ya muziki yenye historia ndefu sana, na iligunduliwa katika mabaki ya ustaarabu wa Banpo mjini Xi'an wyenye historia ya zaidi ya miaka 7,000. Xun ina sauti nzito inayoweza kusikika mbali. Wachina wa zama za kale waliona kuwa sauti ya Xun ni sauti ya majira ya mpukutiko, na inaweza kuwafungulia watu mlango wa kuwasiliana na dunia ya kimaumbile, na kuwafanya watu wafurahie majira ya mpukutiko. Wachina wa zama za kale wanaona majira ya mpukutiko ni majira ya masikitiko, hivyo sauti ya Xun inaweza kuwafanya watu wawe na masikitiko.

    Hivi sasa Xun bado inaendelea kuwavutia watu wengi kwa sauti yake maalumu, na ala hiyo ya muziki inatumiwa katika vikundi vya wanamuziki wa jadi hapa China. Muziki wa Xun uliotungwa na wanamuziki maarufu unaifanya ala hiyo yenye historia ndefu itoe nuru mpya.

    Mbali na Xun, mjini Xi'an kivutio kikubwa zaidi bila shaka ni sanamu za askari na farasi katika kaburi ya mfalme Qinshihuang ambazo zinajulikana kama ni "muujiza mkubwa wa nane duniani". Jumba la makumbusho la sanamu za askari na farasi za kaburi la mfalme Qinshihuang lina upana wa kilomita 37 na sehemu ya katikati ni mji wa Xi'an. Hivi leo, jumba hilo linawavutia maelfu ya watalii kutoka sehemu mbalimbali nchini China na nchi za nje.

    Mwaka 211 kabla ya kuzaliwa Kristo, mfalme Qinshihuang alianzisha nchi kubwa ya muungano baada ya kuyateka madola madogo sita, na kuunda serikali kuu inayoshika madaraka makuu yote. Kabla ya hapo tangu Qinshihuang aanze kuwa mfalme alipokuwa na umri wa miaka 13, alianza kuagiza kujenga kaburi lake. Ujenzi wa kaburi hilo lenye eneo la kilomita 56.25 za mraba uliendelea kwa miaka 38 na watu zaidi ya laki saba walijenga kaburi hilo. Ingawa kaburi hilo ni kubwa sana, lakini lilifichwa vizuri na halijulikana kwa watu hadi ilipofika mwaka 1974. Mwaka huo wakulima wa kijiji cha Shiyang walipochimba kisima ili kukabiliana na maafa ya ukame, waligundua upinde na mishale ya shaba, na sanamu za udongo zilizokuwa ardhini. Idara ya hifadhi ya mali za urithi za utamaduni baada ya kupata habari hii, ilifanya uchimbaji wa kiufundi, na kugundua maelfu ya sanamu za askari na farasi.

    Sanamu hizo za askari na farasi zina urefu kama watu na farasi wa kweli. Ingawa ni nyingi, sanamu hizo zina sura tofauti, hali ambayo inawastaajabisha watu sana. Sanamu hizo ziliwekwa kwenye mistari mbalimbali kama makundi ya wanajeshi walioko tayari kwenda kupambana na maadui. Kikiwa kivutio cha kwanza cha mji wa Xi'an, kila siku jumba la makumbusho la sanamu za askari na farasi za kaburi la mfalme Qinshihuang linatembelewa na watalii wengi. Bw. Antonio kutoka Venezuela baada ya kutembelea jumba hilo alisema,

    "Ni nzuri sana, ni nzuri sana, zinaweza kutukumbusha mambo ya zama za kale."

    Hivi sasa, jumba la makumbusho la sanamu za askari na farasi za kaburi la mfalme Qinshihuang linawapokea watalii karibu milioni mbili kwa mwaka. Kati ya watalii hao, wengi wanatoka nchi za nje. Hata watu wanasema, "kama umeenda kutalii nchini China, na hujatembelea sanamu za askari na farasi za kaburi la mfalme Qinshihuang ni sawa kuwa hujaenda China kutalii."

    Mabaki mengi ya vitu na sehemu za utamaduni yameufanya mji wa Xi'an uwe ni jumba kubwa lisilo na paa la makumbusho ya historia. Lakini kama ukienda huko Xi'an kutalii, huwezi kukosa jumba la kweli la makumbusho ya historia la mkoa wa Shaanxi. Jumba hilo linahifadhi vitu zaidi ya laki 3.7 vya mabaki ya utamaduni ya zama za kale. Vitu hivyo ni pamoja na zana rahisi za mawe zilizotumiwa na mababu wa kale, na vifaa mbalimbali viliyotumiwa na watu miaka 1840 iliyopita, na vitu vingine vya sanaa kama vile vyombo vya shaba nyeusi, sanamu za udongo, vifaa vilivyotengenezwa kwa madini ya dhahabu au fedha, na picha za ukutani.

    Katika jumba la makumbusho historia la mkoa wa Shaanxi, kuna vitu 18 vya utamaduni ambavyo vimethibitishwa kuwa ni hazina za taifa. Kati ya vitu hivyo, viwili vinapigwa marufuku kuoneshwa kwenye maonesho yanayofanyika katika nchi za nje. "kikombe cha ageti chenye umbo la kichwa cha mnyama cha enzi ya Tang" ni moja ya vitu hivyo viwili. Kikombe hicho kiligunduliwa mwaka 1970 katika kijiji kimoja cha mji wa Xi'an. Mwelezaji wa jumba hilo Bw. Xu Xing alisema,

    "Kikombe hicho ni kitu chenye thamani kubwa zaidi katika jumba letu. Kilitengenezwa kwa ageti bora, na tunaona mtu aliyekitumia alikuwa na wadhifa wa juu, huenda alikuwa mfalme au watu wa ukoo wa kifalme. Mwaka 2002, China ilitunga sheria moja ya kupiga marufuku kuoneshwa nje ya nchi kwa baadhi ya mabaki ya utamaduni ya zama za kale yenye thamani kubwa, na kikombe hicho ni moja kati ya mabaki hayo."

    Sehemu kilipotengenezwa kikombe hicho bado haijathibitishwa, lakini wataalamu wana maoni ya pamoja kuwa mtindo wake unatokana na vifaa vya pombe vya nchi za magharibi vya aina ya Laitong. Laitong ni neno la Ugiriki, lina maana ya kuchuja, kwani chini ya kikombe hicho, kuna tundu la kupitisha pombe. Hivyo kinatumiwa kama ni chujio. Watu wa zama za kale wanaamini kuwa kikombe hicho kinaweza kuondoa sumu iliyotiliwa ndani ya pombe. Hivyo kikombe hicho labda ni zawadi ya kitaifa iliyotolewa na nchi ya Asia ya magharibi ya kati kwa mfalme wa enzi ya Tang ya China, na kinaweza kuwa ushahidi muhimu wa mawasiliano kati ya China na nchi za magharibi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako