• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Guangzhou, mji wa milenia wenye opera na muziki maalumu

    (GMT+08:00) 2013-06-24 16:42:17

    Katika sehemu ya kusini mwa China kuna mji mmoja wenye historia ya zaidi ya miaka 2200, unaoitwa Guangzhou. Mji huo uliwahi kuwa mji mkuu wa enzi tatu katika historia, na uliwahi kuwa ni kituo cha kwanza kwa meli za kigeni kutia nanga nchini China, na sasa umekuwa ni mji wa bandari ya biashara na nje iliyo kubwa kabisa na yenye historia ndefu zaidi nchini China. Kwa hiyo mji wa Guangzhou kwa sasa unasifiwa kuwa ni "mji wa biashara wa milenia". Kutokana na hali yake maalumu ya kijiografia na kihistoria, mji wa Guangzhou pia ni sehemu iliyofungua mlango zaidi kwa nje na kuchanganya utamaduni wa China na wa kigeni. Leo katika kipindi hiki tunauzungumzia utamaduni huo maalumu wa Guangzhou.

    Uliyosikia ni lahaja ya kienyeji inayotumiwa sambamba na kichina sanifu, yaani manderin mjini humo, lahaja hiyo inaitwa lahaja ya Guangdong, au kwa kiingereza Cantonese. Lahaja hiyo inayotumiwa kote mkoani Guangdong, lakini ile inayotumiwa mjini Guangzhou ni sanifu zaidi. Lahaja hiyo inatumia maneno mengi ya kichina ya kale, ina sauti tano zaidi kuliko mandarin, na zaidi ya nusu ya maneno yake ni ya kienyeji, kwa hiyo matamshi ya lahaja hiyo yanavutia lakini ni vigumu kujifunza. Hivi sasa, zaidi ya watu milioni 100 duniani wanatumia lahaja hiyo, hasa wakazi wa peninsula ya mto wa Zhujiang, Hongkong, Macau na wachina wanaoishi ng'ambo. Muziki na opera ya kiguangdong yenye historia ya zaidi ya karne moja zote zimeathiriwa kwa kina na lahaja hiyo.

    Opera ya kiguangdong iliyoanzishwa huko Foshan, ni opera ya kienyeji yenye mashabiki wengi zaidi mkoani Guangdong, mpaka sasa imekuwa na historia ya zaidi ya miaka mia tatu. Opera hiyo inayoimbwa kwa lahaja ya kiguangdong, ni opera ya kwanza ya China iliyooneshwa katika nchi za nje. Mwaka 1852, bendi ya opera ya Hongfutang kutoka Guangdong ilifanya maonesho ya opera hiyo mjini San Francisco, Marekani. Opera hii ilikuwa tofauti na opera ya kibeijing iliyooneshwa mara ya kwanza nje ya China mwaka 1930. Miongoni mwa opera za jadi za kichina za aina zaidi ya mia tatu, opera ya kiguangdong ilitambuliwa tarehe 30 Septemba mwaka 2009 na shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa kuwa ni urithi wa kiutamaduni usioonekana duniani, ambayo pia ni opera ya pili ya China kutambuliwa na shirika hilo baada ya opera ya Kunqu.

    Bi. Chen Shaomei amefanya kazi zinazohusiana na opera hiyo kwa zaidi ya miaka 50, na aliwahi kuwa mchezaji, mtungaji na mwongozaji wa opera hiyo. Bi. Chen anaona kuwa Guangzhou ni mji wa bandari wa milenia, umaalumu wa mji huo uliofungua mlango na wenye wakazi wavumilivu pia unaonekana kwenye opera hiyo.

    "opera ya kiguangdong ina sauti nyingi kabisa miongoni mwa opera zaidi ya mia tatu ya China, baadhi ya sauti zinatoka katika opera za mikoa mingine, nyimbo za Hongkong na hata nyimbo za mandarin. Tunaweza kuingiza sauti yoyote kama ikipendwa na watazamaji. Kwa sababu Guangzhou ni mji wa bandari, ulio wazi na wenye uvumilivu, huu ni umaalumu mkubwa wa oprea ya Kiguangdong."

    Mbali na hayo, opera ya kiguangdong pia inatumia nyimbo za kigeni na ala za magharibi kama vile fidla.

    Opera ya kiguangdong inapendwa na watu wengi, hasa wazee kwenye sehemu inayotumia lahaja ya kiguangdong. Kwa kawaida, marafiki wanaweza kuunda bendi yao wenyewe na kucheza opera hiyo katika bustani, au uwanja.

    Mwandishi wetu wa habari alitembelea bendi moja yenye historia ya miaka 31, sasa bendi hiyo ina wasanii 20-30, kila wiki wanakutana mara kwa tatu na kucheza, kuimba pamoja opera hiyo. Mkuu wa bendi hiyo Bw. Jian Guoxin alisema, bendi hiyo imekuwa sehemu isiyokosekana ya maisha yake, wakati bendi hiyo ilipoanzishwa, yeye alikuwa bado kijana, sasa ameshastaafu na kila siku anaendelea kutafuta siri ya opera hiyo.

    "muziki wa pop unakuwa vilevile kama ulivyotungwa. Lakini kila wimbo wa opera ya kiguangdong unaweza kuchezwa kwa mtindo tofauti katika kila maonesho, kwa sababu kuna mitindo mingi ya kuigwa, waimbaji nyota pia wana mitindo yao tofauti, napenda sana mabadiliko hayo."

    Sanaa ya opera ya kiguangdong si kama tu imevutia mashabiki kuunda bendi za kienyeji, bali pia imevumbua muziki wa mtindo wa kiguangdong. Ukitembelea mjini Guangzhou, kila mahali bila kujali ni mtaani, uwanjani, au hotelini, unaweza kusikia muziki wa kiguangdong, na kukuburudisha kwa mtindo wake maalumu wa kienyeji.

    Katika kipindi kirefu cha kihistoria, muziki wa kiguangdong ulichukuliwa nchini hata duniani kuwa ni "muziki wa taifa wa China". Mwaka 1954, muziki wa Guangdong ulisifiwa na mwanamuziki mmoja wa Urusi ya zamani kuwa ni "muziki ulio wazi", yaani ukifumba macho yake, unaweza kupata undani wake akilini mwako mara maja.

    Msemo wa kale unasema, ardhi tofauti inawalea watu tofauti, na lahaja tofauti pia zinaunda utamaduni tofauti. Bw. Tang Kaixuan ni mrithi wa muziki wa kiguangdong ambao ni urithi wa kiutamaduni usioonekana wa China, alitoa mfano akisema, muziki wa Kiguangdong ni kama kitoweo cha kiguangdong, inakubidi uonje polepole kwanza, ndio unaweza kugundua ladha zake tofauti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako