• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbunge wa kujitegemea wa kabila la Berber achaguliwa kuwa kiongozi wa Libya

    (GMT+08:00) 2013-06-26 10:24:33

    Bunge la Libya jana lilimchagua mbunge wa kujitegemea wa kabila la Berber Nuri Abusahmain, kuwa kiongozi mpya wa Libya. Bw. Abusahmain ameshinda kwa kupata kura 96 katika raundi ya pili ya kura kwenye baraza hilo dhidi ya mpinzani wake Al-Sharif-Wafi aliyepata kura 80, ambaye pia anajitegemea, na kufanya apate ushindi mkubwa kwa kundi la makabila madogo. Chama cha kihafidhina na chama cha kiliberali havikuweka wagombea katika uchaguzi huo, ambao umeitishwa baada ya kiongozi wa mwanzo Mohamed Magarief kujiuzulu mwezi uliopita. Bw. Magarief aliondolewa kwa mujibu wa sheria mpya ambayo inapiga marufuku maofisa wa zamani waliokuwa kwenye utawala wa Muammar Gaddafi kushika nafasi serikalini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako