• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0625

    (GMT+08:00) 2013-06-26 16:58:36
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Philp Ng'ang'a Kiarie wa S.L.P 601 Maragua Kenya anasema salamu zangu ziwafikie watangazaji wote pamoja na wasimamizi wa idhaa ya Kiswahili ya Redio China Kimataifa. Pia pongezi ziwafikie wasikilizaji wote walioshinda nafasi mbalimbali na walioshiriki kwenye shindano la chemsha bongo la miaka 45 tangu China na Tanzania zianzishe uhusiano wa kibalozi. Ni furaha kuwa hata watanzania wanapenda kusikiliza vipindi na matangazo ya idhaa ya kiswahiliya CRI.

    Ukweli ni kwamba redio hii inatufurahisha sana sisi wasikilizaji tunaoandika barua kwa vile hamna ubaguzi wa kusoma barua zetu na pia mnazihifadhi na kuziweka hata kwenye matangazo na vipindi vya kwenye tovuti. Kuhusu zawadi za washindi wa nafasi mbalimbali kwenye shindano la chemsha bongo, ni wazi kuwa umewadia wakati ambapo idhaa ya Kiswahili imedhihirisha kuwa uhusiano kati yake na wasikilizaji wake ni wa kunufaishana, kwa mfano wasikilizaji walioshinda cherahani wamepata fursa nzuri ya kuanzisha biashara ndogo ndogo na kuanza kupata mapato ili kukabiliana na wakati huu mgumu, ambapo gharama ya maisha inaendelea kupoanda. Nashukuru sana.

    Nasi tunakushukuru sana msikilziaji wetu Philp Ng'ang'a Kiarie kwa kuendelea kusikiliza matangazo na vipindi vyetu. Redio China China Kimataifa inajali sana wasikilizaji wake na ndio maana huwa inajaribu kutafuta kila njia za kuweza kuwasaidia wasikilizaji wetu hususan kupitia mashindano ya chemsha bongo na kutoa zawadi mbalimbali, ahsante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Mutanda Ayub Shariff wa S.L.P 172, Bungoma anasema Pokeeni salamu za dhati, nikiwafahamisha kuwa nimewamis wote kwa muda, kwani ni muda tangu ninakili barua kwa idhaa ya CRI. Hii ni idhaa iliyoniwezesha kuvuka mito, miamba, mabonde na milima pamoja na ziwa kubwa duniani na vyote vilivyomo ulimwenguni.

    Kando na hayo, mbali na kupata shahada ya maktaba katika chuo cha kitaifa cha ufundi SIGALAGALA, jimbo la Kakamega-Kenya, mkoa wa magharibi. Hivi sasa naelekea kuhitimu tena katika chuo kikuu cha Nairobi (Nairobi University) katika shahada ya meneja wa wafanyikazi wa umma pamoja na masilahi ya wafanyikazi. Wahenga hawakukosea waliposema kimya kingi kina mshindo mkuu.

    Shukran za dhati msikilizaji wetu Mutanda Ayub Shariff kwa barua yako kuhusu maendeleo yako ya chuo, tunakutakia mafanikio makubwa katika masomo na mambo yako kwa ujumla, ahsante sana.

    Barua ya sasa inatoka kwa msikilizaji wetu Juma N. Katala wa S.L.P 452 Bongomela Ndala Tabora Tanzania anasema salamu kwa watangazaji wa redio China Kimataifa na hongera sana kwa kazi zenu nzuri za kila siku za kutuhabarisha taarifa mbalimbali. Mimi ni mzima wa afya njema na ninaendelea kusikiliza redioChinakila siku kupitia KBC.

    Nilifarijika sana na kipindi cha tarehe 19.3.2013 ambacho mlimhoji na kumuelezea mama mmoja wa Kenya aliyekuwa na watoto zaidi ya 20 anaowatunza. Nilivutiwa sana kwa wema na ukarimu na moyo wa mzuri wa imani kwa mama huyo. Maombi yangu ni kuwa mashirika, taasisi na watu binafsi wamsaidie misaada ya hali na mali, ninimani watoto wale wanazidi kukua na wanazidi kuongezeka kwa hiyo mahitaji yao nayo yanazidi kuongezeka.

    Pia ushauri wangu kwa mama huyo ajitahidi kumpata mtu au watu wengine wa kumsaidia endapo tu hatujui ni lini mtu anaweza kufariki. Ila tunamuombea maisha marefu yenye afya njema, lakini umri nao utakuwa kikwazo kwa kuwahudumia watoto hao kama alivyo sasa. Hongereni sana kwa tafiti zenu hizo mbalimbali.

    Tunakushukuru sana msikilizaji wetu Juma N. Katala kwa barua yako, ambayo inaonesha unafuatilia kwa karibu sana vipindi vyetu, tunakupongeza kwa hili. Lakini pia nasi tunampongeza mama huyo kwa moyo wa ujasiri wa kuwakusanya watoto wenye mahitaji na kuamua kuwatunza, kwa kweli hiyo ni hatua nzuri aliyoifikia mama huyo, wahenga wanasemna kutoa ni moyo usambe utajiri. Ahsante sana.

    Mwisho tunawaletea ujumbe tuliyotumiwa na wasikilizaji wetu kupitia tovuti yetu na kwanza ni kutoka kwa Lenusi Kingalu Wa Kihonda S.L.P 24 Morogoro Tanzania anasema katika uchumi na maendeleo tarehe 10/4/013 hii itakuwa faraja na huenda mafanikio kwa nchi za Afrika kwa kufutwa kwa kodi ya bidhaa zake. Na je kila mkoa wa China umejaa viwanda? Maana bidhaa ni nyingi mno kutoka China. Kwani kuna watu ambao hawana kazi kweli katika nchi hiyo? tarehe 11/4/013, matangazo kuhusu siku ya kusafisha makaburi. Inakuwaje kwamba wachina wanaamini kuwa wafu bado wanahitaji magari, nyumba, fedha nk? Salamu Fadhili Mpunji na Pili Mwinyi mlioendesha kipindi hiki.

    Ujumbe wa mwisho unatoka kwa msikilizaji wetu Mogire Machuki baruapepe ni oscarmogire@yahoo.com ujumbe wake unahusu "China yapenda kushirikiana kwa karibu na serikali ya Kenya " anasema Hii ni habari njema kwa Wakenya. China ni rafiki wa dhati wa Kenya na nina imani kuwa urafiki huu ni wa kudumu, Ushirikiano baina ya mataifa haya mawili ni wa kuaminika na wa kunufaishana. Asante China kwa kuitambua serikali mpya ya Kenya.

    Tunawashukuru wasikilizaji wetu wote mliotutumia ujumbe na kutoa maoni yenu kwenye tovuti yetu, na kumjibu Mogire Machuki ni kwamba kwa ujumla kila mkoa una viwanda ila inategemea viwanda vya aina gani, na vilevile wapo watu ambao wamekosa ajira kama ilivyo nchi zote duniani, ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako