Taasisi za fedha nchi ya Tanzania zimeshauriwa kuangalia upya riba ya mikopo zinazotozwa wakopaji, ili kuwainua wananchi badala ya kuwanyonya kifedha.
Akizungumza wakati wa kuzindua huduma mpya za Banki ya Afrika jijini Dar Es Salaam Waziri wa nchi, katika ofisi ya Rais, Bi. Celina Kombani alisema riba ikipunguzwa wateja wa mabenki watachukua mikopo kwa wingi na kuanzisha biashara na pia mabenki kufaidika kutokana na kuongezeka kwa faida kutokana na mikopo.
Bi Kombani anasema mfumo wa riba kubwa umekuwa ukitumiwa na benki nchini kwa hofu ya kupata hasara, jambo ambalo uwaangusha wakopaji kwa kukosa mikopo wakiogopa riba za juu kutoka kwa mabenki
Bi Kombani anasema kama riba itapunguzwa, wafanyakazi wengi wa umma watakopa kwa ajili ya kufanyia shughuli za maendeleo na taasisi hizo zitapata wateja wengi na faida kubwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |