• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjukuu wa Mandela aondolewa katika wadhifa wake wa kikabila

    (GMT+08:00) 2013-07-07 19:47:20

    Mjukuu wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela ameondolewa kwenye wadhifa wake wa kikabila huku ugomvi mkubwa wa kifamilia kuhusu maeneo watakayozikwa watoto watatu wa Mandela ukiendelea kurindima.

    Akithibitisha habari hizo mfalme Zwelibanzi Dalindeyo wa kabila la Thembu ambalo pia ni kabila la Mandela, amesema Mandla Mandela amevuliwa vyeo vyote kwenye kabila hilo kutokana na ugomvi huo. Mfalme huyo amesisitiza kuwa Mandla ambaye ni chifu wa eneo la Mvezo la mkoa wa Cape Mashariki hataruhusiwa kushiriki kwenye mambo ya kikabila hadi atakapoomba radhi.

    Yote haya yanakuja huku Mandela akiwa katika hali mbaya na kuendelea na matibabu ya matatizo ya mapafu kwa wiki ya nne katika hospitali ya magonjwa ya moyo huko Pretoria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako