• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0813

    (GMT+08:00) 2013-08-14 15:42:24
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba ametuletea barua kupitia baruapepe epst01@hotmail.com anasema leo anataka kuzungumzia kuhusu habari ya "China yazitaka pande husika ziiheshimu Afrika na kutimiza ahadi za misaada " anasema kwanza nitoe pongezi zangu za dhati kwa rais Xi Jinping kwa kauli aliyoitoa wakati wa mazungumzo yake na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mjini Beijing.

    Rais Xi Jinping alisema jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuheshimu nia ya Afrika ya kujichagulia njia ya kujiendeleza, kujenga uhusianao wenye usawa na kunufaishana na Afrika na kushirikiana na Afrika kwa lengo la kupata maendeleo ya pamoja, kauli hiyo inaleta faraja kubwa kwa nchi za Afrika ambazo ziko katika jitihada za kujikwamua kutoka katika hali duni za kiuchumi.

    Vile vile hatua iliyofikiwa na nchi ya Ethiopia ya kujiunga na Shirika la Biashara Duniani(WTO) ni nzuri sana, kwani itasaidia kuinua uchumi wa nchi hiyo. Kwa ujumla naipongeza idhaa ya kiswahili ya redio China kimataifa kwa kutujuza habari kemkem kutoka sehemu mbalimbali duniani na zenye mvuto wa kipekee masikioni mwetu sisi wasikilizaji wenu.

    Tunakushukuru sana msikilizaji wetu kwa barua yako ambayo inaonesha kuwa unafuatilia kwa karibu sana matangazo yetu. Kuhusu kauli ya rais Xi Jinping hata sisi pia tunaipongeza kwani inaonesha jinsi gani China inavyolitetea bara la Afrika liweze kujiamulia na kujiletea maendeleo yake bila kupangiwa na nchi nyingine. Ahsante sana.

    Barua ya sasa inatoka kwa msikilizaji wetu Simon Makhanu Mwibale wa S.L.P 387-50200 Bungoma Kenya, naye anasema kwanza kwa heshima na taadhima napenda kuwapa mkono wa pongezi kwa ubora wa hali ya juu wa vipindi na kukidhi haja ya wasikilizaji. Ni vipindi vya kufana sana kiasi cha kufanya mimi kutobanduka redioni. Nianze na kipindi cha jifunze kichina ambacho kinanifurahisha sana na sauti ya wanawake. Hivyo watangazaji wa redio China wanastahili pongezi za dhati, hongera sana kwa kutusomea salamu zetu.

    Nataja tena nikiwa na ushahidi mzuri juu ya vipindi vyenu murua. Mara hii ni kipindi cha uchumi na maendeleo hiki ni kipindi kinachotoa nafasi haswa ya kujua jinsi gani kweli uchumi wa dunia unavyoendelea na hususan China ambayo inasemekana kuwa uchumi wake unaelekea kukua zaidi duniani. Mwisho ningependa kujifunza kichina kupitia CD zenu na magazeti, natumai kuwa ombi langu litapokelewa na mtaniletea kupitia njia ya posta. Shukran za dhati waandaaji wa vipindi vyote, Mungu awe pamoja nanyi.

    Nasi tunakushukuru sana msikilizaji wetu Simon Makhanu Mwibale kwa barua yako, tunapokea pongezi zako kwa mikono miwili, huku tukiahidi kuboresha zaidi matangazo na vipindi vyetu mbalimbali. Pia tunakuomba wewe na wasikilizaji wetu wengine msisite kututumia mapendekezo zaidi, kwani kama mjuavyo idhaa ya Kiswahili inajali mchango na mapendekezo ya wasikilizaj wake, ahsante sana.

    Sasa tunawaletea maoni tuliyotumiwa na wasikilizaji wetu kupitia kwenye tovuti yetu, na kwanza ni msikilizaji wetu Semugenyi Abdu Sulaiman wa S.L.P 3303 Kampala 201 Uganda anasema tunaifurahia Radio China kimataifa kwa kutupasha habari kwa lugha ya Kiswahili kupitia masafa ya 107.3 FM hapa Kampala kituo cha African Bible University Lubowa karibu na mahali petu Entebbe road. Kingine naomba munitumie stickers na ratiba. Nataka na T-shirt kila mtu aione na asikie CRI.

    Naye Manjori anasema Napenda jinsi China inavyo fanya vizuri katika mambo ya kiuchumi

    Maoni ya sasa yanatoka kwa Mogire machuki wa Bogeka Village S.L.P 646, Kisii Kenya anasema vipi CRI, hapa nipo kwenye pekua pekua zangu kwenye ukurasa huu wa CRI. Hapa bila shaka nimefika na huwa napata unafuu na kuhisi vizuri ninaposoma taarifa mbalimbali kwenye ukurasa huu. Asante na kazi njema.

    Tunawashukuru wasikilizaji wetu wote mliotutumia maoni yenu kupitia kwenye tovuti yetu, tunawaomba muendelee kusikiliza matangazo na vipindi vyetu na kuendelea kutoa maoni na mapendekezo yenu, ili tujue wapi pa kurekebisha na wapo ba kuboresha zaidi. Ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako