• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0820

    (GMT+08:00) 2013-08-20 10:29:07
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Paul Mungai Mwangi wa S.L.P 69 North Kinangop Kenya anaanza kwa kusema salamu za dhati wa moyo wangu naomba ziwafikie wasikilizaji, wahariri, watangazaji na wafanyakazi wote wa redio China kimataifa. Nashukuru kurejea tena hewani baada ya kukamilisha kipindi cha mafunzo nchini Marekani. Aidha nawashukuru wapenzi wa salamu walionisalimia japo niliondoka bila kuaga.

    CRI ni stesheni ya kutajika. Vipindi vyake murua vimetayarishwa kitaalamu. Watangazaji mahiri kama vile mama Chen, Pili Mwinyi, Fadhili Mpunji, Fundi Bengo, Caroline Nassoro, Jackob Mogoa, D.J Mosy, Xie Yi na wengineo wote bila kumsahau mkurugenzi wa idhaa ya Kiswahili Han Mei, wote wanakipamba kituo. Pia mashabiki wa salamu, chemsha bongo na sanduku la Barua hawajanitoka fikirani mwangu. Wafuatao ni baadhi yao, Mchana J Mchana, Zuhura Khavere, Kilulu Kulwa, Stephen Magoye Kumalija, Mutanda Ayubu Shariff, Mwanahawa Akhoth, Jim Godfrey, Martin. Y Nyatundo, Jackline Andeyo, Philip Ng'ang'a Kiarie, Joyce Magoye Kumalija, Mbarak Mohamed Abecheri, Ali Khamis Kimani, Okongo Okeya, Ramdhani Khamis, Yaqub Saidi, Mogire Machuki, Bilali Ibrahim, Halima Ijeiza, Mbarouk Msabah, Ras Frans Manko Ngogo, Chacha Matarara, Kepher O. Gichana, Dominic Nduku Muholo na Linet Savai. Anaema nyote nawapa mkono wa kheri na fanaka.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Paul Mungai Mwangi kwa barua yako baada ya kimya kirefu, lakini sasa jibu tumelipata, kumbe ulikuwa masomoni nchini Marekani. Tunatumaini kuwa masomo yalienda vizuri. Pia CRI inakupongeza kwa kuhitimu masomo yako, kwani wahenga walisema elimu ni ufunguo wa maisha pia elimu haina mwisho, ahsante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Adward N'gambi anayetunziwa barua zake na Gideon Musakwa chuo kikuu cha Zambia, Luska zambia anasema napenda kutoa salamu zangu za heri na baraka kwa mwaka huu wa 2013, kwa watangazaji wote wa idhaa ya Kiswahili ya redio China kimataifa. Kwanza namshukuru Mungu kwa kupata nafasi hii ambayo nimepewa ili nipate kuandika barua hii. Kwa ujumla napenda kuwasalimu watangazaji kutokana na kazi yenu kubwa kwa kutuletea mambo yanayotokea duniani pamoja na nchini China Mungu awe pamoja nanyi.

    Pia nimepatwa na utashi wa kuandika barua hii kutokana na kutoweza kuwasiliana nanyi kwa takriban mwaka mzima na nusu. Hii ni kwasababu ya tatizo la kiafya kwa wakati wote huo, hivyo ningependa kuomba msamaha. Tatizo kubwa ni ugonjwa wa TB ukanifanya nisiweze kutembea wala kukaa hivyo nililazimika kulazwa hospitali kwa miezi saba.

    Kwanza kabisa tunapenda kukupa pole msikilizaji wetu Adward N'gambi kwa kusumbuliwa na ugonjwa kwa muda mrefu, tunakuombea kwa Mungu upone haraka. Lakini vilevile tunakushuru sana kwa barua yako ingawa ni muda mrefu umepita hujawasiliana nasi, lakini sasa tumejua tatizo ni nini, pole sana na ahsante sana.

    Mwisho tunawaletea maoni tuliyotumiwa na wasikilizaji wetu kupitia kwenye tovuti yetu, kwanza ni msikilizaji wetu Grace wa S.L.P 72703 anasema jamani wandugu vipi tamthilya ya Doudou na mama wakwe zake? Tunaomba ianze upya. Kama haiwezekani tunaomba iuzwe katika DVD. Tutanunua sana. Naomba mzingatie maana ina mafunzo na inaburudisha akili.

    Naye Lameck anasema Jitihada zifanyike habari zitufikie kwa muda muafaka.

    Na nwisho ni maoni kutoka kwa msikilizaji wetu Alimasi Baraka Fizi wa DRC anasema ujumbe wake unahusu habari ya "Kampuni ya China yaanza ujenzi wa reli ya kisasa nchini" Fanya kazi China wewe tuna kusubiri hata Congo DRC. wengine hatujaona hata njiya ya reli. karibu kwetu.

    Tunawashukuru sana wasikilizaji wetu wote mliotutumia maoni yenu kupitia kwenye tovuti yetu, tunawaomba muendelee kusikiliza matangazo na vipindi vyetu, ili muweze kututumia ujumbe na mapendekezo yenu ambayo yatasaidia kuboresha zaidi matangazo yetu kwa ujumla, ahsanteni sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako