• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama cha masoko ya dhamana Afrika Mashariki chaweka mipango muhimu soko la hisa

    (GMT+08:00) 2013-08-08 20:31:05

    Kampala-Chama cha masoko ya dhamana Afrika Mashariki kimeafikia juu ya mipango mitano muhimu ambayo yatapelekea muungano kamili na maendeleo ya masoko ya hisa katika kanda. Chama hicho kinaundwa na watendaji wakuu wa masoko ya hisa ya Nairobi , Tanzania , Uganda , Rwanda na mtendaji mkuu wa Shirika la Central Depository and Settlement Corporation la Kenya .

    Mipango hiyo mitano ilijadili viwango vya kikanda vya mifumo ya madalali,ambayo chama hicho kinasema itafanya shughuli zote za kikanda katika kompyuta.

    Mfumo huo pia utapunguza hatari ya biashara ya dhamana zilizotajwa kwenye masoko ya kikanda, kuongeza imani ya wawekezaji na kuwezesha upatikanaji zaidi kupitia biashara ya kwenye intaneti.

    Aidha mfumo huo utaboresha uadilifu wa mifumo ya biashara ya hisa na kuwezesha upatikanaji zaidi wa masoko ya dhamana.

    Mipango mengine iliyojadiliwa ilikuwa ni pamoja na mfumo wa uhamishaji uhamishaji,mfumo ambao utaleta jukwaa la kusaidia upatikanaji na ulipaji wa dhamana atika masoko ya kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako