• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hazina ya Taifa Kenya kutenga shilingi bilioni 2.7 kwa ajili ya kupunguza ada za uunganishaji umeme

    (GMT+08:00) 2013-08-15 20:22:56

    Hazina ya Taifa nchini Kenya itaipatia kampuni ya umeme ya Kenya shilingi bilioni 2.7 katika muda wa miezi mitatu ijayo ili kuiwezesha kampuni hiyo kurudia ada za zamani za kuwaunganisha wateja wapya katika gridi ya taifa ya umeme.

    Hii inatarajiwa kuizuia kampuni hiyo kupata hasara na kuelekeza fedha ambazo kampuni hiyo ilisema zilitengwa kwa ajili ya mahitaji mengine ya kibiashara ili kutoa ruzuku kwa wateja wapya.

    Serikali ya Kenya inafanya utafiti ili kutathmini gharama za uunganishwaji umeme.Utafiti huo unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwezi huu.

    Fedha hizo kutoka kwa serikali zitakuwa ahueni kwa wateja wapya ambao walifungiwa kutopata uunganishwaji wa umeme kutokana na viwango vya ada vilivyowekwa na kampuni ya umeme ya Kenya Power tangu mwezi Januari mwaka huu.

    Hivi sasa kampuni hiyo itarudia mara moja ada za zamani za shilingi 35,000 kwa unganishaji umeme wa awamu moja kutoka shilingi 60,000.Pia itaiwezesha kampuni hiyo kulipisha shilingi 49,000 kwa uunganishaji wa awamu tatu kutoka shilingi 70,000.

    Kampuni hiyo ilirejelea ada za zamani tarehe 12 mwezi Agosti na wateja ambao walitozwa ada za 60,000 na 70,000 kabla ya tarehe hiyo hawatafidiwa.

    Dar es salaam Tanzania :Precision Airways yazongwa na madeni ya zaidi ya shilingi milioni 51.

    Kampuni ya ndege ya Precion Air inakabiliwa na ukosefu wa fedha za kuendeleza biashara yake na huenda ikafungwa iwapo itashindwa kulipa dola milioni 51.2 inazodaiwa na idara mbalimbali.

    Mwenyekiti wa kampuni hiyo Michael Shirima amethibitisha hali hiyo na kueleza kuwa wanatafuta fedha kutoka idara tofauti pamoja na serikali ya Tanzania ili kujinasua kutokana na mkosi huo.

    Tatizo kuu la kampuni hiyo ni kuwa inakabiliwa na madeni makubwa kutoka kwa benki za kibiashara nchini Tanzania na sasa wameiomba serikali kujitolea kuwa wadhamini dhidi ya madeni hayo.

    Shirima anasema madeni ya kampuni hiyo yaliongezeka kufuatia kununuliwa kwa ndege saba za thamani ya dola milioni 136 kutoka ufaransa na Italy mwaka 2007.

    Ndege hizo zilitarajiwa kuregesha fedha hizo zilizotarajiwa kuongeza hisa za kampuni hiyo japo matokeo ya biashara yalikuwa kinyume na matarajio.

    Kampuni ya Precision inashirikiana na shirika la ndege la Kenya Airways ikiwa na hisa za asilimia 43 na huku KQ ikishikilia hisa za asilimia 41.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako