• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Russia kukuza zaidi uhusiano kati yao

    (GMT+08:00) 2013-08-17 20:09:05

     

    China na Russia zimekubaliana kuweka juhudi za kuhimiza uhusiano kati yao. Akizungumza mjini Sochi baada ya kukutana na mjumbe wa taifa la China Yang Jiechi, rais Vladimir Putin wa Russia amesema amekubaliana na rais Xi Jinping wa China kutoa juhudi zote kwa ajili ya kuhimiza uhusiano kati ya Russia na China katika kiwango cha juu zaidi. Amesema Russia ina nia na imani ya kushirikiana na China ili kutekeleza mpango wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, kudumisha maingiliano ya karibu na ya ngazi ya juu, kuimarisha ushirikiano halisi na mawasiliano na ushirikiano katika mambo ya kimataifa, na kulinda amani na utulivu wa kikanda na kimataifa kwa pamoja.

    Rais Putin pia amesema anatarajia kuwa rais Xi Jinping atahudhuria mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 20 utakaofanyika mwezi ujao nchini Russia ambapo watakutana na kubadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili na masuala makuu ya kimataifa na kuhimiza ushirikiano kati ya China na Russia katika miradi mikubwa.

    Kwa upande wake, Bw. Yang Jiechi amesema, marasi wa nchi hizo mbili wametoa mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati yao walipokutana Machi mwaka huu. Nchi hizo mbili zimekuwa zikitekeleza kwa juhudi makubaliano yaliyofikiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako