• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0827

    (GMT+08:00) 2013-08-27 18:38:12
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Philip Ng'ang'a Kiarie wa S.L.P 601 Maragua Kenya, anaanza kwa kusema kwanza salamu zangu ziwafikie watangazaji na wasimamizi wote wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio China Kimataifa. Naomba kuchukua fursa hii ili kuwajulisha kwamba nimepokea zawadi za vitabu sita vya jifunze kichina pamoja na bahasha mbili zilizolipwa gharama.

    Ni jambo la kutia moyo na kuwapa wasikilizaji fursa nzuri ya kujifunza kichina kupitia redio, huku wakiwa wanasoma moja kwa moja kupitia kwenye vitabu hivyo. Kwa kuzungungumzia zaidi vitabu hivyo vina vidokezo vingi vya utamaduni wa watu wa China kwa mfano kidokezo kuhusu michezo ya Olimpiki ya Beijing iliyofanyika kuanzia tarehe 8 hadi 24 Agosti mwaka 2008, hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa China kuandaa michezo ya Olimpiki ya majira ya joto.

    Mpangilio wa vitabu hivyo unapendeza zaidi kwani kila mwanzo wa somo moja kuna marudio ya maneno ya somo lililopita, nimefurahishwa sana na vitabu hivyo ambavyo vimenifikia wakati muafaka, nashukuru. Mbali na hayo vitabu hivyo vimeandikwa kwa lugha mbili yaani kichina na Kiswahili vilevile kuna matamshi ya maneno kwa pinyini. Waafrika na wachina watapata fursa nzuri ya kujifunza lugha za Kiswahili na kichina na kunufaishana.

    Idhaa ya Kiswahili ya redio China Kimataifa imepiga hatua kubwa katika kutuelimisha sisi wasikilizaji lugha ya kichina na utamaduni wa wachina, nawapongeza wana CRI kwa kuchukua muda wao mwingi kueneza lugha na utamaduni wa China. Mwisho ombi langu ni kuwa matangazo ya masomo yote 68 ya kuwa nasi jifunze kichina ikiwezakana yawe yanarudiwa mara kwa mara ahsante sana.

    Nasi tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Philip Ng'ang'a Kiarie kwa barua yako, pia tunafurahia kusikia kuwa vitabu pamoja na CD za kujifunza kichina zinakusaidieni sana katika kuijua lugha ya kichina, lakini mbali na lugha pia mnaweza kuufahamu utamaduni wa China ambao una historia ndefu sana. Kuhusu kurudia mara kwa mara vipindi vya kuwa nasi jifunze kichina tutajitahidi kwani tunajua tukifanya hivyo tutawasaidia hata wale ambao ndio kwanza wanajifunza, ahsante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Aaron Thomas wa S.L.P 1805 Kisii Kenya anasema kutokana na mashauri ya wasikilizaji wa CRI tunapenda uongezwe muda wa kupata matangazo ya CRI, hii ni kufuatia ubora wa matangazo yenu ambayo yanaburudisha mashabiki wengi wa Afrika Mashariki na kwingineko. Wasikilizaji wengi wanapenda kujiunga na CRI lakini shida ni kuwa hawajajisajili kupitia kwenye fomu zenu. Pia nashukuru kwa zawadi ambayo nilipata kutunukiwa kwa kuwa mshindi wa pili katika mashindano ya maonesho ya Shanghai.

    Tunakushukuru sana msikilizaji wetu kwa barua yako fupi. Kuhusu matangazo tumejitahidi kuongeza muda na ndio maana tunarusha matangazo yetu mara tatu kwa siku. Ahsante sana.

    Sasa ni zamu ya msikilizaji wetu Gulam Haji Karim wa S.L.P 504 Lindi Tanzania, anasema natoa pongezi kwa watangazaji na watayarishaji wote wa vipindi kwa kutuletea matangazo murua kabisa. Baada ya CRI kufanya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwake, redio hii imekuwa ikivuma sana.

    CRI imefanya mengi sana ya kujivunia, kutokana na vipindi vyake kuwa ni vya kuvutia, kuelimisha na kuburudisha. Mfano mzuri ni kipindi cha salamu zenu na jifunze kichina vina wasikilizaji wengi, kwa kweli ni dakika 5 tu lakini tunanufaika na kujua neno moja au mawili. Mimi kwa upande wangu sijafaidika kwani kichwa changu kigumu, hata hivyo najua maneno ya kusalimiana kama vile Ni hao, na xiexie yaani asante. Nawapongeza wale wanaoendelea kujifunza. Ahsante sana.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Gulam Haji Karim kwa barua yako, kwanza tunakupa pole kwa kushindwa kujifunza kichina kwa urahisi, lakini hata hivyo tunakushauri uendelee hivyo hivyo kidogokidogo hatimaye utapata maneno mengi ya kichina ingawa mwanzo ni mgumu, ahsante sana.

    Mwisho tunawaletea ujumbe kutoka kwa msikilizaji wetu Carl Pistorious D'souza baruapepe yake ni Jacksonkvicent23@gmail.com anasema makala hii ni nzuri lakini nataka kujua je nyinyi mnawezaje kuongea kiswahili wakati nyinyi ni wachina?

    Tunakushukuru msikilizaji wetu Carl Pistorious D'souza kwa ujumbe wako, kuhusu swali lako kwamba tunawezaje kuongea Kiswahili na sisi ni wachina, ni kwamba nasi tumejifunza Kiswahili na vilevile kwenda nchi kama Tanzania na Kenya ili kufanya mazoezi zaidi ya kuongea na kujua wenyeji wanaongea kwa mtindo gani, ndio maana wafanyakazi wa redio China Kimataifa idhaa ya kiswahili wote wanaongea Kiswahili, ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako