• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jiping atafanya ziara katika nchi za Asia ya Kati na kufafanua sera ya mambo ya nje ya China kwa kanda hiyo

    (GMT+08:00) 2013-08-27 18:11:28

    Wizara ya Mambo ya Nje ya China leo imesema rais Xi Jiping atafanya ziara katika nchi nne za Asia ya Kati na kuhudhuria mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 20 (G20) na mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai. Wakati wa ziara yake, rais Xi atafafanua sera kamili kuhusu mambo ya nje inayofuatwa na serikali ya awamu mpya ya China kwa Asia ya Kati, na kutoa mapendekezo mapya ya kuimarisha ushirikiano kati ya China na nchi mbalimbali za kanda hiyo. Kuhusu kama mkutano wa wakuu wa China na Japan utafanyika wakati wa mkutano wa G20, wizara ya mambo ya nje imesema, hakuna msingi wa kufanyika kwa mkutano huo.

    Tarehe 3, Septemba, rais Xi Jinping ataanza ziara ya nchi nne za Asia ya Kati, hii itakuwa mara ya kwanza kwa rais Xi kutembelea nchi za kanda hiyo. Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Cheng Guoping anasema (sauti 1) "rais Xi atatembelea nchi hizo za Asia ya Kati, na wakati wa mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, rais Xi atakutana na mwenzake wa Tajikistan na kusaini makubaliano ya ushirikiano katika sekta za mafuta, gesi ya asili, mawasiliano barabarani, upashanaji habari, uwekezaji na utamaduni. Aidha, rais Xi atatoa hotuba kwenye Chuo Kikuu cha Nazarbayev nchini Kazakhstan, ambapo atafafanua sera ya mambo ya nje ya China kwa kanda ya Asia ya Kati."

    Rais Xi pia atahudhuria mkutano wa 13 wa baraza la wakuu la nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai utakaofanyika tarehe 13, Septemba nchini Tajikistan. Baada ya miaka 12 toka jumuiya hiyo ianzishwe, mwaka jana ushirikiano halisi kati ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo ulianza kuendelezwa kwa kasi. Bw. Cheng amesema mkutano huo utajadili hatua za kuimarisha zaidi ushirikiano huo, na kubadilishana maoni na kuratibu msimamo kuhusu masuala makubwa ya kimataifa na kikanda.

    Kwa mujibu wa mwaliko wa rais Vladimir Putin wa Russia, rais Xi pia atahudhuria mkutano wa nane wa wakuu wa nchi wa kundi la nchi tajiri na zile zinazoinukia kiuchumi duniani la G20 utakaofanyika tarehe 5 na 6 huko St. Petersburg. Katika mazingira ya kufufuka kwa uchumi wa dunia ulio dhaifu na kuongezeka kwa kiasi kikubwa kwa utoaji wa sarafu, ikiwa ni utaratibu muhimu wa uongozi wa uchumi wa dunia, mkutano huo utafuatiliwa zaidi. Mkutano wa G20 wa mwaka huu wenye kauli mbiu ya "ukuaji na ajira" utakuwa na ajenda nne za ukuaji wa uchumi wa dunia na utulivu wa mambo ya fedha, nafasi za ajira na uwekezaji, maendeleo endelevu na biashara ya kimataifa. Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw Li Baodong ameeleza matarajio ya China kuhusu mkutano wa G20.

    (sauti 2) "Cha muhimu ni kutekeleza uamuzi wa Shirika la Fedha Duniani kuhusu mageuzi ya mgawanyo wa kura katika shirika hilo, na kumaliza kwa wakati mageuzi hayo na duru jipya la ukaguzi wa mgawanyo wa kura; kuongeza uwakilishi wa masoko mapya na nchi zinazoendelea katika mashirika ya fedha ya kimataifa; kuimarisha usimamizi wa mambo ya fedha ili kuufanya mfumo wa mambo ya fedha uwe wa kutegemeka, uhudumie na kuhimiza maendeleo ya uchumi, na kujenga mfumo huo uwe tulivu na wenye uwezo wa kukabiliana na hatari."

    Mbali na ajenda kuhusu mambo ya uchumi, kinachofuatuliwa kwenye mkutano huo, ni marais wa nchi gani watakutana na rais Xi, haswa kama rais Xi Jinping atakutana na waziri mkuu wa Japan. Hivi karibuni, Japan inatoa habari ikisema waziri mkuu wa Japan anatafuta fursa ya kuongea na rais Xi wakiwa wamesimama. Bw. Li amesisitiza kuwa kwa mujibu wa msimamo wa Japan kuhusu historia na uhusiano kati ya China na Japan, hakuna sababu ya msingi kwa viongozi wa China na Japan kukutana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako