• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Brazil ajiuzulu kufuatia wasiwasi wa kidiplomasia na Bolivia

    (GMT+08:00) 2013-08-27 18:37:03

    Waziri wa mambo ya nje wa Brazil Antonio Patriota amejiulu jana kufuatia kuongezeka kwa hali ya wasiwasi na Bolivia baada ya seneta wa nchi hiyo Rogar Pinto kukimbia nyumbani kwao akisaidiwa na mwanadiplomasia wa Brazil.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais, Patriota alijiuzulu baada ya kukutana na rais Dilma Rousseff, na nafasi yake amechukuliwa na mkuu wa tume ya Brazil katika Umoja wa Mataifa Luiz Alberto Figueiredo. Awali mwanadiplomasia wa Brazil Eduardo Saboia aliyekuwa mjini Laz Paz, amesema alifanikiwa kumsafirisha Pinto, ambaye ni mpinzani wa rais wa Bolivia Evo Morales hadi nchini Brazil ijumaa iliyopita baada ya kuzuiwa kwa miezi 15 katika ubalozi wa Brazil nchini Bolivia.

    Pinto alikuwa akitafutwa na serikali ya Bolivia kwa mashtaka ya ufisadi na mengineyo. Serikali ya Bolivia imesema tukio hilo linaweza kuharibu uhusiano kati ya nchi hizo mbili majirani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako