• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afisa wa Benki ya China asema makubaliano kuhusu hazina ya dharura yakaribia kufikiwa

    (GMT+08:00) 2013-08-27 18:38:02

    Afisa wa ngazi ya juu wa Benki kuu ya China amesema nchi za BRICS zinakaribia kufikia makubaliano ya kuanzisha Mpango wa Hazina ya Dharura CRA ndani ya jumuiya hiyo.

    Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, naibu gavana wa Benki ya Watu wa China Yi Gang, amesema katika mkutano mkuu wa tano wa BRICS uliofanyika mwezi Machi nchini Afrika Kusini, viongozi walikubaliana kuweka Mpango wa Hazina ya Dharura kwa kianzio cha dola bilioni 100 za kimarekani. Mpango huo utasaidia nchi hizo kupunguza shinikizo la muda mfupi, kusaidia kila upande na kuimarisha utulivu wa kifedha. Amesema makubaliano zaidi kuhusu CRA yatafikiwa wakati viongozi wa nchi hizo watakapofanya mkutano usio rasmi katika kipindi cha mkutano wa kundi la nchi 20 ambao umepangwa kufanyika Septemba 5 na 6 huko St. Petersburg.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako