• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0903

    (GMT+08:00) 2013-09-25 16:34:27
    Leonard Bernard Maganja wa S.L.P 6870 Dar-es-salaam, Tanzania anaanza kwa kusema nashauri radio China kimataifa ianzishe vipindi ambavyo vitaelimisha na kuelezea masuala muhimu ambayo yatachochea maendeleo na mahusihano kati ya watu wa China na Afrika. Mfano kipindi kitakachozungumzia masuala ya elimu, sanaa(filamu, muziki, uchoraji nk) vijana, utalii na utamaduni. Vipindi hivi vitazalisha na kuamsha mapenzi ya waafrika kwa nchi ya China na watu wake.

    Pia ili kushindana na radio nyingine duniani, itakuwa vyema siku zijazo mkafikiria kuanzisha matangazo ya televisheni. Pia kutembeleana na radio China kushiriki maonyesho ya shughuli zenu za utangazaji katika maonyesho ya sabasaba hapa Tanzania, yatasaidia wazungumzaji wengi kuijua na kuifahamu radio China kimataifa. Haya ndio maoni yangu kwa radio niipendayo radio China kimataifa.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Leonard Bernard Maganja kwa barua yako fupi lakini imejaa ushauri. Kwa upande wa vipindi vyetu tunajitahidi kugusia kila upande ikiwemo elimu utamaduni vijana, utalii, muziki, uchumi n.k. lakini kuna jambo moja ulilopendekeza la kushiriki kwenye maonesho ya sabasaba ili tuoneshe shughuli zetu redio China kimataifa, kwa kweli jambo hilo limetugusa sana na tunafikiri ni njia moja wapo ya kuitangaza redio yetu, hivyo tutakaa chini na kujadili kwa kina ahsante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Choma Wa Choma wa S.L.P 108 Mwamkulu Mpanda Tanzania. Naye anasema hongereni radio China kimataifa, kwanza nawavulia kofia watangazaji, pamoja na mkurugenzi wa redio China kimataifa, mko juu sana mimi ninakipenda kipindi cha uchumi na biashara, maana hapo elimu ni ya kutosha sana, nawapa pongezi kwa moyo wenu wa kujituma, na kutangaza biashara na uchumi wenu, na kuleta bidhaa mbalimbali, mfano huku nimeona mashine za kuvuna mpuga. Hapo wakulima wa mwamkulu nikiwemo na mimi choma massanja choma, hatuna tabu tena ya usumbufu wa kuvuna mpuga asateni sana radio China. Pia mimi ni shabiki wa CRI. Lakini nimechukua mazuri kupitia vipindi mbalimbali. Nakuchukua elimu tosha sana, kwanza radio China ikianza kutangaza tu kama ninakula naacha ili nisikie vizuri kwa makini na uhakika.

    Pia nawashukuru sana CRI kuwatembelea wadau wa Kenya hapo shukurani. Nauliza, Je radio China itatutembelea lini nchini Tanzania nawaomba mje Mpanda Katavi Tanzania. mje mjionee hifadhi ya wanyama na ziwa Tangayika kuna samaki wazuri sana ahsante sana.

    Nasi tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Choma Wa Choma kwa barua yako, kwanza tunakupongeza kwa kuwa shabiki wetu mkubwa wa matangazo na vipindi vyetu. Kuhusu kutembelewa huko Katavi wafanyakazi wetu wakipata safari ya Tanzania, wanaweza kuja huko siku moja. Lakini inakuwa vigumu sana kukuahidi moja kwa moja kwani kazi zinatuzonga sana, mpaka wakati mwingine inakuwa vigumu kutembelea klabu za wasikilizaji wetu, hata hivyo tutajitahidi.

    Mwisho tunawaletea ujumbe tuliotumiwa na wasikilizaji wetu kupitia kwenye tovuti yetu na kwanza ni msikilizaji wetu Samson Kyanzi wa S.L.P 245 Musoma Tanzania anasema mataifa ya magharibi yanajaribu kueneza sera zao za demokrasia je ni kweri bila demokrasa nchi haiendi?

    Naye Kipkoech victor Langat baruapepe yake ni Victorkipkoech13@gmail.com anasema ningependa kujifunza kichina kwa kina na naomba sana kwa unyenyekevu wangu munipe taratibu ya kufuata.

    Msikilizaji wetu Kira anasema ujumbe wake unahusu "UN yatoa mwito wa kusimamisha vita nchini Syria katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan. Viongozi waumini wawape ushauri kwa kipindi hiki cha kuomba msamaha kwa yasiyo mpendeza mwenyezi mungu

    Bakary BKB naye anasema ujumbe unahusu "Watu 162 wamethibitishwa kufariki katika tetemeko la ardhi China mimi nawaomba wasijenge majengo yenye zaidi ya ghorofa tatu.

    Eliasante Marema baruapepe yake ni elisantemarema@ yahoo.com anauliza ni vipi naweza kupata tamthilia ya doudou kwenye dvd tafadhali naomba nijibiwe kwenye e-mail yangu hapo juu kwenye anuani yangu.

    Tunawashukuru wasikilizaji wetu wote mliotutumia ujumbe kupitia tovuti yetu, lakini kumjibu Eliasante Marema kuhusu tamthilia ya Doudou na mama wakwe zake, bado hatujatoa kwenye DVD tutakapotoa tutawajulisha mashabiki wote ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako