• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa wakuu wa G20 kufuatilia ongezeko endelevu

    (GMT+08:00) 2013-08-28 18:17:11

    Mkutano wa nane wa wakuu wa kundi la nchi 20 utafanyika tarehe 5 na 6 mwezi Septemba huko St.Petersburg nchini Russia. Katika mazingira ya sasa ambapo uchumi wa dunia hauna nguvu kubwa ya kufufuka na imani ya watu kuhusu soko inaathiriwa sana na msukosuko wa madeni, kundi la nchi 20 linalochukua asilimia 90 katika thamani ya jumla ya uzalishaji duniani, litachukua hatua gani za kukusanya nguvu, kuhimiza ongezeko endelevu la uchumi wa dunia na kulinda utulivu wa fedha za kimataifa, suala hili linafuatiliwa sana na nchi mbalimbali.

    Kauli mbiu ya mkutano huo iliyotolewa na Russia ambayo ni nchi mwenyekiti wa mkutano huo, ni "ongezeko na nafasi za ajira".

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Li Baodong jana alisema, China inatarajia mkutano huo utaonesha moyo wa wenzi wa ushirikiano wa kundi la nchi 20, na kuzitaka nchi mbalimbali zichukue sera za kiuchumi za kuwajibika, na kuimarisha uratibu na ushirikiano wa sera za uchumi mkubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako