• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mratibu wa mkutano wa G20 wa Russia asema ukuaji endelevu ni kazi kuu ya wajumbe wa mkutano

    (GMT+08:00) 2013-09-04 18:41:15

    Mratibu wa mkutano wa kundi la nchi 20 wa Russia Bibi Ksenia Yudaeva amesema ukuaji endelevu utakaokuwa imara ni kazi kuu ya uchumi wa kundi la nchi 20. Bibi Yudaeva amesema ingawa tishio la kifedha katika nchi za Ulaya na nchi nyingine limepungua katika miaka ya hivi karibuni, kazi muhimu kwa nchi zilizoendelea na zinazoendelea bado haijatimizwa, ambayo ni kurudi kwenye njia ya ukuaji mkubwa ulio endelevu. Kwa mujibu wa Yudaeva sababu ya kimsingi ya kudorora kwa ukuaji ni kutokana na ukosefu wa vyanzo vipya vya ukuaji.

    Katika mkutano wa kundi la nchi 20 utakaofunguliwa kesho huko St. Petersburg, wajumbe watajadili hatua za kukabiliana na kudodora kwa ukuaji wa uchumi, kuhimiza maendeleo ya muda mrefu, kuandaa sera za kusaidia kukidhi mahitaji ya watumiaji na uwekezaji wa fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako