• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China amaliza ziara nchini Turkmenistan

    (GMT+08:00) 2013-09-04 21:01:40

    Rais Xi Jinping wa China leo amemaliza ziara yake nchini Turkmenistan, na kuelekea St.Petersburg, Russia kuhudhuria mkutano wa wakuu wa G20. Kabla ya kuondoka Turkmenistan rais Xi Jinping na rais Gurbanguly Berdymukhamedov wa Turkmenistan walihudhuria hafla ya kukamilika kwa hatua ya kwanza kwa ujenzi wa mradi wa shamba la gesi la Galkynysh uliojengwa na kampuni ya mafuta na gesi ya China.

    Shamba la gesi la Galkynysh ni shamba kubwa la pili la gesi duniani, malimbikizo ya gesi iliyogunduliwa kwa sasa kwenye eneo hilo ni mita za ujazo bilioni 4 hadi bilioni 6. Shamba hilo la gesi ni kituo muhimu kwa Turkmenistan kuuza gesi yake kwa nchi za nje, pia ni sehemu muhimu ya ushirikiano wa gesi kati ya China na Turkmenistan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako