• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China afika Saint Peterburg kuhudhuria mkutano wa kundi la nchi 20

    (GMT+08:00) 2013-09-05 10:24:28

    Rais Xi Jinping wa China jana aliwasili mjini Saint Petersburg, Russia ili kuhudhuria mkutano wa nane wa wakuu wa kundi la nchi 20 utakaofanyika huko kuanzia leo hadi tarehe 6. Mkutano huo utajadili masuala mbalimbali kuhusu hali ya uchumi na mambo ya fedha duniani, uwekezaji, biashara, maendeleo na mageuzi ya mfumo wa kimataifa wa mambo ya fedha. Mbali na kuhudhuria mkutano huo, rais Xi Jinping pia atakutana na viongozi wanaohudhuria mkutano huo, wakiwemo rais Vladimir Putin wa Russia na rais Barack Obama wa Marekani, na kuhudhuria mkutano usio rasmi wa viongozi wa nchi za BRICS yaani Brazil, Russia, India China na Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako