• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuyumbishwa kwa mkutano mkuu wa G20 kunavuruga matumaini ya jumuiya ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2013-09-05 18:23:52

    Tishio la Marekani la kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Syria limeongeza hatari ya kuyumbisha mkutano mkuu wa G20 utakaofanyika hivi karibuni, ambao unapaswa kufuatilia mambo ya uchumi duniani.

    Ni dhahiri kuwa Russia ambayo ni nchi mwenyeji wa mkutano huo imeweka masuala ya kuhimiza ongezeko la uchumi na kuongeza nafasi za ajira kuwa mada kuu za mkutano huo, lakini rais wa Marekani Barack Obama atatumia fursa ya mkutano huo kufikisha suala la Syria kwenye mkutano huo, akitafuta uungaji mkono kwa mpango wake wa hatua za kijeshi dhidi ya Syria.

    Kwanza, Obama anapaswa kuzishawishi nchi washirika wa Marekani zisizotaka vita zikubali uamuzi wake, ambayo ni kazi ngumu kwake.

    Bunge la Uingereza liliamua kuizuia serikali ya Uingereza kushiriki kwenye hatua za kijeshi za Marekani dhidi ya Syria, ambalo ni pigo kubwa kwa Obama. Rais wa Ufaransa Francois Hollande anayeunga mkono hatua za kijeshi, alibadilisha msimamo wake na akasema kuwa uamuzi huo utajadiliwa kwenye bunge kabla ya kuanzisha mashambulizi. Kwa Ujerumani, viongozi wake hawajatoa msimamo dhahiri kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utakaofanyika tarehe 22 Septemba.

    Ya pili, Obama analazimika kukabiliana na aibu ili aweze kutafuta fursa ya kuzungumza na rais wa Russia juu ya suala la Syria.

    Kutokana na sera wazi ya Putin kuhusu suala la Syria, na upinzani mkali wake dhidi ya hatua za kijeshi, Obama atakuwa na kazi ngumu kumshawishi kwa nini Marekani inataka kuchukua hatua hiyo kukabiliana na hatari ambayo wapiganaji wa Jihad watadhibiti Syria.

    Ya tatu, Obama atazungumza na viongozi wengine kwenye mkutano huo. Hatua za kijeshi zitakazoongozwa na Marekani peke yake zitatoa ishara ya hatari duniani kwa kuwa hatua hizo bado hazijapata idhini ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon amesema bayana kuwa ni lazima idhini itoke kwa Baraza la usalama, akitangaza kuwa itachukua muda wa wiki kadhaa kwa wachunguzi wa Umoja huo kuthibitisha waliohusika na matumizi ya silaha za kemikali.

    Mkutano mkuu wa G20 ni baraza muhimu kwa viongozi kutafuta hatua nyingi zaidi za kukuza uchumi wa dunia wakati ambapo uchumi huo unakosa nguvu ya msukumo, na athari ya msukosuko wa fedha duniani unaendelea bila kupunguza nguvu yake.

    Kwa hiyo, itasikitisha kama Marekani inajaribu kuyumbisha mkutano huo kutokana na maslahi yake, wakati ambapo jumuiya ya kimataifa inatafuta na kusubiri hatua za kukuza uchumi zenye ufanisi kutoka kwa nchi kubwa duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako