• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi Jinping ajadili na rais wa Russia kuhusu uhusiano na masuala ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2013-09-05 19:09:19

    Rais Xi Jinping wa China leo amekutana na mwenzake wa Russia Vladimir Putin huko Saint Petersburg nchini Russia kabla ya mkutano wa G20.

    Kwenye mkutano huo, Rais Xi amesema, anafurahia kuona nchi mbili China na Russia zimefanya juhudi kubwa ya kutekeleza miradi zaidi ya 50 ya ushirikiano katika sekta 16 tangu mkutano wao uliopita. Kwa upande wake, rais Putin amesema Russia inapenda kuimarisha uratibu na ushirikiano na China katika kuhimiza mkutano wa G20 kupata matokeo katika masuala ya ongezeko la uchumi wa dunia, mageuzi ya mfumo wa kifedha ya kimataifa, na kulinda maslahi ya nchi zinazoibuka kiuchumi duniani.

    Pia ameeleza nia yake ya kubadilishana maoni na rais Putin, kuhusu masuala yanayofuatiliwa na pande zote mbili . Huu ni mkutano wa pili kati ya marais hao wawili ndani ya miezi sita baada ya rais Xi kufanya ziara nchini Russia mwezi Machi.

    Habari nyingine zinasema, rais Xi leo pia amekutana na rais Dilma Rousseff wa Brazil na rais Christina wa Argentina kwa nyakati tofauti.

    Rais Rousseff amesema, hivi sasa hali ya ufufukaji wa uchumi wa dunia bado ni polepole sana, nchi zinazojitokeza kiuchumi zikiwemo China na Brazil zinatakiwa kuimarisha mawasiliano na uratibu, kuzihimiza kwa pamoja nchi husika kuchukua sera za kiuchumi za kuwajibika, na kusukuma mbele mageuzi ya mfumo wa fedha wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako