• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 20 wafunguliwa St. Petersburg

    (GMT+08:00) 2013-09-06 14:08:48

    Mkutano wa 8 wa wakuu wa kundi la nchi 20 ulifunguliwa jana alasiri huko St. Petersburg, Russia, ambapo wakuu wa nchi wajumbe wa kundi hilo, na viongozi wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia wanahudhuria mkutano huo, wakijadili suala la "kuhimiza ongezeko la uchumi na ajira".

    Rais Vladmir Putin wa Russia aliendesha mkutano huo, na kusema kwenye mkutano wa wakuu wa mwaka jana uliofanyika Los Cabos, viongozi wa nchi mbalimbali walithibitisha hatua mbalimbali za kukabiliana na msukosuko wa fedha duniani, ambazo zimefanya kazi nzuri. Rais Putin alisema,

    "Kwa ujumla, kundi la nchi 20 limethibitisha kuwa lina uwezo wa kutatua masuala nyeti. Kutokana na hatua nzuri, hivi sasa hali ya uchumi wa dunia imeboreshwa. Matatizo makubwa yametatuliwa kwa kiasi fulani au kudhibitiwa."

    Rais Putin pia alisema, hivi sasa kazi muhimu ni kuufanya uchumi wa dunia urudi katika hali ya kuendelezwa kwa njia endelevu na kwa uwiano, lakini hatari ya kimfumo na msingi wa msukosuko wa uchumi bado havijatatuliwa, na uchumi wa dunia unakabiliwa na hatari mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako