• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Marekani wakutana kwa mara mbili ndani ya miezi mitatu

    (GMT+08:00) 2013-09-06 18:43:26

    Rais Xi Jinping wa China na rais Barack Obama wa Marekani wamekutana leo mjini St. Petersburgļ¼ŒRussia na kujadili uhusiano kati ya nchi hizo mbili na masuala yanayofuatiliwa na pande zote mbili.

    Rais Xi Jinping amesema uhusiano kati ya China na Marekani umedumisha mwelekeo wa maendeleo ya kasi. Amesema China na Marekani zimeendelea kuimarisha uhusiano wao wa kijeshi na kuendeleza mawasiliano na ushirikiano katika masuala ya kikanda na kimataifa.

    Kwa upande wake rais Barack Obama amesema Marekani na China zimepata maendeleo katika ushirikiano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na kuimarisha uhusiano wa kijeshi.

    Hii ni mara ya pili kwa marais hawa wawili kukutana ndani ya miezi mitatu. Mwezi Juni, marais hawa walikutana huko Annenberg estate, jimbo la California nchini Marekani, ambapo walikubali kujenga uhusiano wa aina mpya kati ya nchi hizo mbili ambao utaepuka makabiliano na mgogoro wa zamani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako