• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping apendekeza kujenga ukanda wa kiuchumi wa "Njia ya Hariri"

    (GMT+08:00) 2013-09-07 20:10:54

    Rais Xi Jinping wa China ambaye yuko ziarani nchini Kazakhstan ametoa hotuba muhimu iitwayo "kuimarisha urafiki na kujenga mustakabali mzuri kwa pamoja" katika Chuo Kikuu cha Nazarbayev, ambapo amesifu sana urafiki wa jadi kati ya China na Kazakhstan, kufafanua sera za ujirani mwema, urafiki na ushirikian zinazotekelezwa na China kwa nchi za Asia ya Kati, kupendekeza kujenga ukanda wa kiuchumi wa "Njia ya Hariri" kwa kutumia utaratibu mpya wa ushirikiano, na kuifanya kazi hiyo iwe ya kuwanufaisha watu wa nchi mbalimbali zilizoko katika kanda hiyo.

    Rais Xi Jinping amesema ili kuufanya uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi mbalimbali za Ulaya na Asia uwe wa karibu zaidi, ni lazima kuendeleza kwa kina zaidi ushirikiano, na kuzifanya nafasi za maendeleo ziwe kubwa zaidi, nchi mbalimbali zinaweza kujenga kwa pamoja ukanda wa kiuchumi wa "Njia ya Hariri", na kuanzisha ushirikiano mkubwa wa kikanda hatua kwa hatua. Ameeleza kuwa nchi mbalimbali zinatakiwa kuimarisha kazi ya kuratibu sera, kurahisisha njia za kufanya mawasiliano, kuzifanya shughuli za biashara zifanyike bila matatizo, kuyafanya mzunguko wa fedha uendelee vizuri, na kuwafanya watu wa pande husika waongeze mawasiliano kati yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako