• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0910

    (GMT+08:00) 2013-09-10 15:35:54
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba baruapepe yake ni epst01@hotmail.com anaanza kwa kusema wahenga walisema maji ni uhai, msemo huo ukiutathimini unaweza kuona kuwa una umuhimu mkubwa sana katika jamii yoyote ile au taifa lolote lile lenye vyanzo vya maji. Leo nimeweza kuangalia tovuti ya CRI ambayo imesheheni habari lukuki zenye manufaa makubwa kwa wasomaji wa tovuti hiyo, kwani nimeweza kusoma habari nzuri sana ambayo imeangazia Ziwa Victoria ambalo ni kubwa kuliko maziwa yote barani Afrika, pia ni ziwa la pili kwa ukubwa duniani.

    Ni ukweli usiopingika kuwa hatua zanatakiwa kuchukuliwa kulinusuru ziwa victoria ambalo linakabiliwa na hatari ya uchafuzi, magugu maji na kupungua kwa maji kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Ni jukumu la kila mwana jamii ambaye anaishi pembezoni mwa ziwa hilo kuhakikisha utunzaji bora wa mazingira hayo.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Epafara Stanley Deteba kwa barua yako fupi, lakini imebeba ujumbe mzito. Kama ulivyosema kweli maji ni uhai, kwani binaadamu anategemea maji kwa asilimia nyingi sana, hivyo tunapaswa kutunza na kuvienzi vyanzo vyote vya maji ikiwemo maziwa, mito n.k. ahsante sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Choma wa Choma au Kamanda wa mashambulizi ya S.L.P 108 Mwamkulu Mpanda Tanzania anasema katika kipindi cha leo cha Sanduku la barua, kwanza napenda kuwapa salamu zenu watangazaji, wasikilizaji na wachambuzi wa vipindi na matangazo mbalimbali, kuanzia salamu zenu, cheche zetu, na jifunze kichina. Mimi nimejifuza mengi sana kupitia radio china. Kwa vipindi vyenu sitawasahau Pili Mwinyi na Fundi Bengo na DJ Moss. Na mkurugenzi wa radio China kimataifa, mana mnaelimisha watu kwa makini na uhakika.

    Mimi naipogeza redio yetu ya China mana nikisema yenu nitakosea. Ni yetu wasikilizaji. Mana mimi ni shabiki wa redio China. Ahsanteni sana Mungu awabariki mpaka shetani ashagae. Pia nawashukuru sana kwa kupata ukurasa wa facebook mana hapo nitakua natuma ujumbe bila shida na usumbufu. hongera CRI China.

    Nasi tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Choma wa Choma kwa barua, pia tunapokea pongezi zako kwa mikono miwili. Lakini kikubwa ni kukuomba uendelee kusikiliza matangazo yetu na vipindi na kuweza kutoa maoni na mapendekezo yako ahsante sana.

    Sasa tunawaletea maoni tuliyotumiwa na wasikilizaji kupitia kwenye tovui yetu kanza ni msikilizaji wetu Priscus Tarimo wa S.L.P 210 anasema jamani wanao sema Rais Nelson Mandela atolewe ile mashine inayomsaidia kupumua hawamtakii maisha mema, hivyo namuomba Mungu ampe maisha marefu hapa duniani pamoja na wale wanao mchukia awasaidie ili kurudia hali ya kawaida.

    Benego anasema ujumbe wake unahusu "Moto uliozuka kwenye Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, Kenya. Mimi naomba ulinzi uimarishe Kenya ili kujiepusha na majanga

    Naye lenusi kingalu baruapepe yake ni kingalu@yahoo.com anasema mikate ya taguo yaweza kuliwa na watu wote au maalumu kwaajili yao tu watu wa jixi? swali kuna viwanda vingapi vinaoka mikate ya taguo. na ikitokea mikate hiyo haipo hao wafanyabiashara wa Anhui wanategemea chakula gani katika safari zao?

    SIMON baruapepe yake ni ntelyas09@gmail.com anasema uhuru wa kupata habari ni haki ya kila mtu nawatakieni kazi njema katika kuhabarisha jamii duniani, mimi ni mwanafunzi chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam nchini TANZANIA.

    Mwisho ni ujumbe kutoka kwa Ngida Ngereza Laizar ujumbe wake unahusu Ripoti ya majimbo yalioathirika sana na Ukimwi Kenya. Ndugu zangu wa duniani tupunguze ngono zembe kuwa na mmoja inatosha.

    Tunawashukuru kwa dhati wasikilizaji wetu wote mliotutumia ujumbe na maoni kupitia kwenye tovuti yetu, lakini tunapenda kuungana na Ngida Ngereza kuhusu janga la Ukimwi, nasi tunasema watu wanapaswa kuwa makini kwa kutulia na mpenzi mmoja, na kwa wale waliopo kwenye ndoa kuhakikisha wanalinda ndoa zao, kwa kufanya hivyo tutapunguza maambukizi mapya ya Ukimwi. Mwisho tunawaomba muendelee kusikiliza matangazo na vipindi vyetu ahsanteni sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako