• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0917

    (GMT+08:00) 2013-09-25 16:34:27
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Erick Rutta barua yakepepe ni fokotoz2004@yahoo.com anaanza kwa kusema Mimi nipo Tanzania yaani hapo zamani nilikuwa nikisikiliza sana redio hii moja kwa moja. Sasa hata kwenye tovuti siwezi tena kwa kuwa ni gharama sana kwa huku Tanzania. Ombi langu au maoni yangu ni kwanini na nyinyi msitafute radio washirika kama wengine ili muweze kuwafikia watu wengi zaidi.

    Kuhusu vitu mbalimbali hivi vinasomeka vizuri mtandaoni bila shida. Tumieni hiyo e-mail kunitumia hizo mita band ili niweze kuwapata kwa masafa marefu. Naomba swala hili msipuuzie ni muhimu mimi ni mtu makini na nadhani na nyinyi mtakuwa watu makini. Nawatakia kazi njema. Hata facebook nipo jaribuni kuniadd ili tuwe pamoja.

    Sasa hivi hili swala la kuanza kutumia radio washirika na hapa Tanzania mtaanza lini au ndo mmetutenga kama watoto yatima. kaa mkijua mlikuwa na wasikilizaji wengi sana hapa Tanzania. na watanzania ni kama ndugu na wachina. mimi nashangaa sana mmeshindwa kufanya jitihada zozote ili kuweza kupata radio washirika ili tuweze kuwapata na sisi vizuri zaidi. Hiyo anuani hapo juu ni kwa ajili ya vijarida vyenu tulivyokuwa tukivipata hapo zamani naomba sana turudishe undugu wa usikilizaji kama zamani nimezikumbuka sana barua kwa kweli mimi ni mkosoaji mkuu kutoka kanda ya kati kama kawaida yangu huwa sifichi ovu hata siku moja nitasema tu nikipata fursa. nawatakia kazi njema.

    Naye msikilizaji wetu Emmanuel Meng'anyi Mseti wa S.L.P 376 Tarime-Mara-Tanzania anasema namuunga mkono Bwana Edward Kabamba wa S.L.P 9060 Manyara, kwa maoni yake ya kutaka vipindi vya CRI tuwe tunavisikiliza kupitia radio za nchini Tanzania, haswa TBC taifa itatusaidia saana kuliko kuitegemea KBC ambayo inatufikia huku Tarime kwa shida, muda mwingi tunavikosa vipindi vingi. Hongereni uongozi wa redio China kwa kazi nzuri mnayoifanya, na Mungu awabariki.

    Tunakushukuru sana wasikilizaji wetu Erick Rutta na Emmanuel Meng'anyi Mseti kwa barua zenu, ambazo mmejaribu kueleza kinaga ubaga yale uliyonayo moyoni. Sisi tunafurahi tukipata watu wanaotueleza ukweli. Lakini kuhusu malalamiko yenu kwa kweli sisi kwa upande wetu tumejitahidi vya kutosha kuwahimiza wahusika wa TBC na CRI, sasa utaratibu unaendelea ili kuhakikisha matangazo yanarusha katika TBC taifa, lakini kwa kweli hatujuia matatizo yako wapi, tunawaomba wasikilizaji wetu wanaweza kutuelewa, tusubiri pamoja basi, ahsanteni sana.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Wilifred Thuita wa S.L.P 421 Igahga Uganda anasema Nihao mimi ni shabiki mpya kutoka Kenya lakini sasa hivi niko Iganga Uganda. Nimefurahia vipindi vyenu zuri sana hua napenda kipindi cha cheche zetu sana. Pia bila hata kusahau kipindi cha jifunze kichina na walimu wetu Moses na Han mei, Mungu awabariki sana. Pia napenda kutuma salaamu zangu kwa mashabiki wote wa radio China kimataifa. Mimi ni shabiki mpya kutoka mwaka 2004 Mungu awe nanyi xeixei.

    Tunakushuru msikilizaji wetu Wilifred Thuita kwa barua yako fupi, kwa vile wewe ni shabiki mpya tunakukaribisha kwa mikono miwili uendelee kusikiliza vipindi vyetu na kutoa maoni ahsante sana.

    Mwisho tunawaletea maoni tuliyotumiwa na wasikilizaji wetu kupitia kwenye tovuti yetu na kwanza ni msikilizaji wetu Amini Abdul wa Dar es salaam anasema namwombea mzee wetu Mandela apone haraka.

    Naye Edwin wa S.L.P 1550 Iringa Tanzania anasema nawapongeza na kuwatakia kila kheri za kutupa habari motomoto.

    Alan wa Buja baruapepe yake ni nabdukar@yahoo.fr anasema naanza kwa kusema yakwamba nampenda sana Fundi Bengo; hata na Pili Mwinyi, Moses, Mogoa na kipindi chao cha "SALAM ZENU" na kile kinachofuata hadi matangazo ya kiswahili kuisha. Nina hamu nimuone Bengo hata kwenye Picha. Ntaskiya raha saaaaana.

    Tunawashukuru kwa dhati wasikilizaji wetu wote mliotutumia maoni yenu kupitia kwenye tovuti yetu. Kwanza tunapenda kupokea pongezi zenu, pia tunaungana na Amini Abdul kumuombea mzee Mandela apone haraka. Mwisho tunawaomba wasikilizaji wetu muendelee kusikiliza matangazo na vipindi vyetu ili muweze kutoa maoni na mapendekezo zaidi ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako