• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 0924

    (GMT+08:00) 2013-09-25 16:34:31
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Simon Peter Michael wa Shule ya sekondari Sengenya S.L.P 166 Nanyumbu Masasa Tanzania, anaanza kwa kusema mimi nimechelewa kupokea zawadi kwasababu nilikuwa nje ya nchi kwa kipindi cha miezi minane, hivyo kutokana na kuishi mbali na Dar es salaam ningeomba yafanyike mambo yafuatayo, kugawa simu kwaajili ya mawasiliano baina yenu pamoja nami, kama kuna shughuli ambazo serikali ya China inafanya hapa Tanzania tunaomba tupewe kipaumbele, hata kuajiriwa kwenye makampuni inapobidi. Tunasikia ujio mbalimbali wa ujumbe kutoka China lakini hatushirikishwi kwasababu tumesahaulika.

    Nakumbuka shindano hili lilikuwa na tiketi moja tu ya kwenda China, tunaomba mkitoa tena shindano muongeze idadi ya tiketi, ikiwa ni pamoja na maswali kutuma kwenye anuani za posta, hii itarahisisha. Mwisho nawatakia kazi njema na kutekeleza hayo ambayo nimeyaelekeza, ahsante sana.

    Tunakushukuru sana msikilizaji wetu Simon Peter Michael kwa barua yako ambayo umejaribu kutoa maoni na mapendekezo yako kuhusu utaratibu wa chemsha bongo, lakini tukianzia na chemsha bongo kutuma kwenye sanduku la posta itakuwa vigumu kwani kama mnavyofahamu kawaida barua zinachukua hata mwezi kufika huko. Na kuhusu kushirikishwa au kuajiriwa kwenye kampuni pia inategemea na uwezo wa kufanya kazi fulani, kwani si rahisi kwa kampuni yoyote ile duniani kuajiri mtu bila ya kuwa na utaalamu wa kazi husika, na suala la tiketi huwa hatutoi moja ingawa ni nafasi maalumu lakini washindi wanakuwa kuanzia watatu, ahsante sana.

    Sasa ni zamu ya msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba wa shule ya sekondari Nanga S.L.P 108 Igunga Tabora Tanzania, anasema mimi ni mzima wa afya na naendelea kutegea sikio matangazo yenu. Kama kawaida nikiwa katika makazi mapya mkoani Tabora huku nafundisha masomo ya historia na Kiswahili. Matangazo ninayapata kwa uzuri kupitia masafa mafupi bila ya matatizo yoyote. Pokeeni wingi wa pongezi wafanyakazi na watangazaji wote wa idhaa ya Kiswahili redio China kimataifa, kwa kweli kazi yenu ni nzuri sana na inavutia, hongera mama Chen, Pili, Jackob na wengineo nasema hivi mko juu!!!!pia naomba mnitumie vitabu vya jifunze kichina ili niweze kujifunza zaidi lugha hiyo.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba kwa barua yako. Kwanza tunapenda kupokea pongezi zako ahsante sana. Kuhusu vitabu vya kujifunza kichina tayari tumeshaongea na wahusika na utatumiwa ili uweze kujifunza kwa raha kichina, lakini pia usikose kusikiliza kipindi cha kuwa nasi jifunze kichina pia kitakusaidia sana. Ahsante sana

    Mwisho tunawaletea maoni tuliyotumiwa na wasikilizaji wetu kwenye tovuti yetu na kwanza ni Kija Mudanga wa Tanzania anasema ndugu zangu habari zenu ni nzuri sana japo ni fupifupi hivyo naomba muwe mnazirefusha para ili tuendelee kuwapata kwa uzuri zaidi. asanteni

    Khalifa Iddi Juma wa S.L.P 73226-00200 Nairobi Kenya anasema napenda kuwashukuru sana kwa kazi yenu mzuri sana ya utangazaji. mimi ni shabiki wa CRI idhaa ya Kiswahili na nimerudi sasa baada ya miaka nyingi hii ni baada ya masomo yangu sasa niko nanyi. Pokeeni salamu zangu za dhati-ahsanteeeni.

    Renatuc Kimario hakusema wapi yupo lakini anasema angeomba wachina waendelee kuwekeza barani Afrika kwa wingi ili waafrika tuondokane na umasikini ambao unatukabili

    Salum Mauya wa S.L.P 54 Pingalame Kongwa Dodo anasema ni kwamba kwa mjini matangazo yanapatikana vizuri kwa vijijini hatuyapati kabisa hasa maeneo ya mkoa wa Dodoma.

    Tunawashukuru wasikilizaji wetu mliotutumia maoni kwenye tovuti yetu tunawaomba muendelee kusikiliza zaidi matangazo na kuleta maoni na mapendekezo. Kuhusu kutopatikana vizuri kwa matangazo ni kutokana na kuwa bado hatujaanza kurusha matangazo yetu nchini Tanzania hayo mnayopata ni kutoka Kenya, ahsanteni sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako