Watu wasiofahamika wamerusha maguruneti kwenye makazi ya kamanda wa kikosi cha usalama wa taifa, Wissam Ben Hamid, yaliyopo mjini Benghazi jana jioni. Hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa kuwa wakati wa shambulizi hilo, hakukuwa na mtu yeyote ndani ya nyumba hiyo.
Inaaminika kuwa watu waliofanya shambulizi hilo ni wa kabila la ofisa wa jeshi la Libya, Ahmed Mustafa Al Barghati, aliyeuawa mbele ya nyumba yake na kundi lililokuwa na silaha mapema jana.
Vyanzo vya habari vinasema, inadaiwa kuwa kamanda Hamid anahusika na mauaji hayo.
Benghazi, kitovu cha mapinduzi yaliyomwondoa madarakani kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi, umeshuhudia mauaji na milipuko ya mara kwa mara dhidi ya viongozi wa kijeshi waliofanya kazi kwenye utawala wa Gaddafi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |