• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • barua 1105

    (GMT+08:00) 2013-11-05 17:50:05
    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Arthur Kabugu ambaye ametutumia baruapepe akmathenge@yahoo.com Kenya anaanza kwa kusema natumai hapo CRI Beijing mu wazima wa afya na mwaendelea vyema na shughuli zenu za kuandaa vipindi murua vya CRI. Bila shaka miye ni mzima wa afya na pia ninaendelea vyema na shughuli zangu huku nikipata wasaa wa kusikiliza CRI kupitia Idhaa ya taifa KBC Redio. Miye ningali ninayafuatilia matangazo ya CRI yenye manufaa zaidi.

    Hivi karibuni nilifurahishwa sana kwa jinsi China ilivyomkaribisha Rais Uhuru Kenyatta kwa heshima na taadhima alipofanya ziara rasmi hapo nchini China. Pia kwa msaada wa kifedha kutoka mfuko wa hazina ya China kwa ajili ya nchi ya Kenya. Hilo ni jambo la kupongezwa sana. Upande wa tamthilia ya Doudou na mama wakwe zake inaporushwa hewani kupitia KBC TV ni kipindi kizuri sana ingawa sijapata kukifuatilia vyema kutokana na muda ambao huletwa hewani saa 8.00 (nane) Jumapili ambapo mara nyingi huwa kanisani.

    Ombi langu ni kwa KBC TV, nafasi ikipatikana kipindi hicho kiwe kikirejelewa saa za jioni au usiku katika siku yoyote ili wengi wa watazamaji wapate fursa ya kukitazama bila ya wasiwasi wowote. Nashukuru wasikilizaji wa CRI ambao wamekuwa wakinitumia salamu za mara kwa mara kama vile Ras Franz Manko Ngogo. Ningependa kuwataarifu kuwa salamu zao ziko njiani na ninatumai zikifika zitapeperushwa hewani kupitia idhaa hii ya CRI. Kwa ujumla vipindi ni murua kabisa.

    Mwisho kabisa, ningependa kuwataarifu Redio CRI kuwa tayari nimepokea jarida la DARAJA LA URAFIKI likiambatanishwa na kadi za salamu na bahasha zilizolipiwa. Nashukuru sana kwa Jarida hilo maridadi sana. Nimesoma makala mbalimbali k.v. Hotuba aliyotoa Rais Xi Jinping kwenye kituo cha kimataifa cha mikutano cha Mwalimu Nyerere cha Tanzania, Mwislamu kutoka Tanzania anayejitolea kutoa huduma msikitini, Shairi la Bw. Mutanda Ayubu Shariff lenye kichwa Mola wape amani Tana River, Imani za Jadi na Jinsi ya kupika chakula cha Kichina Gong BaoJi Ding. Nimefurahia makala hayo. Na ninatumai CRI mtazidi kuniletea Jarida hilo ili nikanufaika na kufahamu mambo mbalimbali yanayohusu China na Afrika. Kila la kheri.

    Tunakushukuru kwa dhati msikilizaji wetu Arthur Kabugu kwa barua yako ambayo umezungumzia mambo mbalimbali. Ila kuhusu ziara ya rais Kenyatta hata sisi wachina pia tumefurahia sana kwani tunajua hiyo ndio njia ya kuimarisha ushirikiano na urafiki kati ya nchi zetu, ahsante sana.

    Barua ya sasa inatoka kwa msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba baruapepe yake ni epst01@hotmail.com anasema nianze kwa kusema hivi nchi ya China inastahili pongezi na kuungwa mkono katika mpango wa utekelezaji wa kudhibiti uchafuzi wa hali ya hewa, jambo hilo ni zuri sana, hasa ukiangalia nchi nyingi zimekuwa na tatizo kubwa la uchafuzi wa hali ya hewa.

    Kimsingi hewa inapochafuliwa madhara makubwa huweza kutokea, hasa ikiwa ni matatizo ya kiafya na maradhi mbalimbali kuibuka, nchi ya China ni darasa tosha la kujifunzia kwa nchi nyingine duniani kote ili ziwe na mikakati madhubuti ambayo italeta tija katika jamii. Kwa mfano China imeweka malengo kuwa ifikapo mwaka 2017, magari yanayotoa moshi mwingi yatazuiwa, hii ni kwa sababu yanachangia kwa kiwango kikubwa katika uchafuzi wa hewa. Mimi binafsi naitakia kila la heri serikali ya China ili iweze kufikia malengo yake ya kudhibiti uchafuzi wa hewa, hongereni sana kwa kuwa na mpango mzuri.

    Kwanza tunakushukuru sana msikilizaji wetu Epafra Stanley Deteba kwa barua yako, kwa kweli kama ulivyosema hivi sasa hapa China kuna kampeni ya kupambana na uchafuzi wa hewa. Ndio maana serikali imeweka sheria ya magari kutembea kwa namba maalumu barabarani, pia viwanda vinavyozalisha kidogo vinafungwa na kuhamasisha watu kuhusiana na madhara ya uchafuzi wa hewa. Ahsante sana.

    Mwisho tunawaletea ujumbe tuliotumiwa kupitia kwenye tovuti yetu kwanza ni Yusuph Lyela anasema nawashukuru kwa kutuletea habari motomoto.

    Na Reginald baruapepe yake reginaldpeter@ymail.com anasema nimetembelea radio yenu nimefurahi kuona imeandikwa kwa kiswahili, ila mnahitaji marekebisho kidogo asante sana.

    Tunawashukuru sana wasikilizaji wetu wote mliotuma ujumbe kwenye tovuti yetu, lakini tukimjibu msikilizaji wetu Reginald ni kwamba lugha ya kichina na Kiswahili zina maneno tofauti hivyo baadhi ya wakati kunakuwa na ugumu wa kutafuta maneno halisi, tunatumai kuwa mtatuelewa asante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako