Mtafiti wa ofisi ya uchumi wa jumla ya idara ya utafiti wa mambo ya maendeleo katika baraza la serikali la China Bw. Zhang Liqun leo amesema, kama China inataka kuliwezesha soko lifanye kazi muhimu zaidi katika mgawanyo wa maliasili, ni lazima kubainisha majukumu ya serikali.
Mkutano wa tatu wa kamati kuu ya 18 ya Chama cha Kikomunisti cha China ulifungwa jana hapa Beijing, na kutoa taarifa kuhusu kuendeleza kwa kina mageuzi kwa pande zote. Bw. Zhang Liqun anaona kuwa, sasa mageuzi ya China yameingia katika kipindi cha kihistoria cha kupiga hatua kubwa ili kupata maendeleo makubwa halisi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |