Ripoti iliyotolewa na Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO inasema, kiwango cha bei za chakula duniani kwa mwaka 2013 kilipungua kidogo, lakini bado ni kubwa. Takwimu za bei ya chakula zinaonyesha kuwa, wastani wa kiwango cha bei ya chakula duniani kwa mwaka jana ulikuwa 209.9, ingawa kiwango hiki kilipungua kidogo kuliko mwaka 2012, lakini mwaka jana bado ni miongoni mwa miaka yenye kiwango cha juu cha bei ya chakula tangu takwimu hizo zilipoanza kurekodiwa.
Kutokana na mavuno ya nafaka ya mwaka 2013, bei ya nafaka isipokuwa mchele, na bei za sukari na mafuta ya kupikia zilipungua, lakini bei ya maziwa na nyama ilipanda. Mwanauchumi mmoja wa FAO amesema mahitaji makubwa ya chakula chenye protini nyingi yalisababisha ongezeko la jumla la bei ya chakula.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |